Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Mwisho wa utawala wa chama cha siasa - CCM katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikuwa iwe wakati wa u Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete (2005 - 2010). Ukacheleweshwa kwa kitambo kidogo lakini maandalizi muhimu yakafanyika chini yake.

Kwa ulaghai na kwa udanganyifu wa kidola ktk uchaguzi mkuu wa 2015, wakaponea chupuchupu, wakaendelea kupumua.

Akamtengenezea njia Rais Hayati John P. Magufuli. Akaja na kauli za uharibifu na ubinafsi kama; "utawala wa CCM ya Magufuli" na "Tanzania ya Magufuli"

Huyu akaharibu mifumo ya utendaji ndani ya chama chake. Akaharibu pia mifumo ya utendaji ndani ya Serikali. Na kweli nchi hii ikawa "CCM na Tanzania ya Magufuli kwelikweli" isiyojali sheria wala katiba ya nchi.

Hakuweza kuelewa kuwa UOVU haujawahi kuishinda HAKI. Hakuwa kujua kuwa GIZA halijawahi kuitawala NURU.

Sasa tunaye mwanamama, Samia Suluhu Hassan aliyerithi mikoba ya uharibifu ya kichama na kiserikali ya Mwendazake John P. Magufuli.

Huyu ndiye alama ya mwisho ya anguko la Chama Cha Mapinduzi - CCM na utàwala ktk JMT. Ndiyo inaweza kuwa mwisho wa muungano laghai wa 1964 kati ya zilizokuwa nchi huru mbili za Tanganyika na Zanzibar.

Huyu atakuwa Rais wa kwanza mwanamke kutawala Tanzania na ndiye atakuwa Rais wa mwisho toka CCM kuiongoza Tanzania na ndiyo mwisho wa maisha ya Chama Cha Mapinduzi - CCM.

Alama za majira na nyakati ziko wazi sana kuhusu uthibitisho wa hoja hii:

1. KIFO CHA RAIS JOHN P. MAGUFULI

Sijadili kifo chake kilivyokuwa na sababu zake. Lakini ningependa kila mtu afahamu kuwa si cha bahati mbaya. Ni "call" muhimu, kwamba, tuko mwisho na Tanzania na Watanzania wanakwenda kuanza MAJIRA na NYAKATI mpya kabisa katika nchi yao.

Mwenye akili na asome na kufahamu haya.

2. UJIO WA RAIS WA JMT MWANAMKE

Si kawaida. Hakujiandaa. Hakudhani kuwa atakuwa. Haijalishi tunalionaje. Lakini ni tukio lenye kusudi maalumu ktk utawala wa nchi hii. Hakukubalika kwa kirahisi na kwa haraka ndani ya "deep state" na ndani ya CCM kwa sababu ya "conflict of interests" kati ya makundi mbalimbali.

Hawakumwona kuwa anaweza. Zipo sababu nyingine kama nitakavyoeleza hapa chini.Haya hayakutokea kwa bahati mbaya. Lipo kusudi na linakwenda kutimizwa sawia kitambo si kirefu.

3. UDHAIFU WA KATIBA YA JMT KUHUSU TRANSITION OF POWER IWAPO RAIS ALIYEKO MADARAKANI ANAKUFA AU KUKOSA UWEZO WA KUONGOZA NCHI:

Unaanza na upatikanaji wa "mgombea mwenza" ambaye automatic huwa Rais wa nchi mara litokeapo tukio la kifo au incumbent president kushindwa kutimiza wajibu wake kama inavyoelezwa na katiba ya JMT ya 1977.

Ukweli wa hili umethibitishwa na kifo cha John P. Magufuli na harakati za nani awe Rais badala yake. Udhaifu huu wa kikatiba siyo wa bahati mbaya. Ni ili kusudi la Mungu litimie na litatimia.

4. TANZANIA BARA KUONGOZWA NA RAIS MZANZIBARI WA UPANDE WA PILI WA MUUNGANO:

Hili linaweza na siku zote huonekana kuwa mwiko kuandikwa na kusemwa. Lakini ili tupone, ni sharti lijadiliwe kwa UKWELI na UWAZI. Hili haliko sawa. Halijakaa sawa. Haliatendei haki Watanganyika.

Na kiuhalisia, chanzo chake ni ASILI YA MUUNGANO mwenyewe. Kwamba, muungano kati ya nchi huru hizi mbili Tanganyika na Zanzibar, asili yake si watu au wananchi wenyewe. Huu ni muungano ulioasisiwa na viongozi kwa manufaa ya kisiasa ya viongozi wenyewe.

Ndani ya Chama kinachoongoza serikali (CCM) hawakubaliani na hili. Nje ya CCM wengi wetu, hatukubaliani na hili...

Tanganyika (Tanzania Bara) ina population kubwa sana ya karibu au zaidi ya watu 60,000,000. Zanzibar sehemu ya pili ya Muungano ina population ya watu wasiozidi 2,000,000.

Kuwa na kiongozi mkuu wa nchi kutoka Zanzibar halafu atawale Tanganyika, it is absolutely not right and unacceptable.

Unaweza kulazimisha na kudanganya watu kwa nyakati fulani. Lakini haiwezi kuwa hivyo nyakati zote.

Sababu hii ndiyo ilitaka kuleta mtafuruku wa kutaka kuvunjwa kwa katiba ya JMT na kisha muungano kwa baadhi ya Watanganyika ndani ya serikali na CCM kutaka kukataa kumpa u Rais mama Samia S. Hassan sawasawa na katiba inavyoelekeza.

Hii ni ishara (signal) muhimu ya udhaifu wa Muungano huu na unaithibitisha hoja hii sawia.

Sasa hili haliko kwa bàhati mbaya. Lipo kwa kusudi maalumu tangu wakati ule ili kutimizwa kwa mwisho wa majira na nyakati hizi na kuanza majira na nyakati mpya za utawala wa nchi hii.

5. KUIBUKA KWA KASI TENA YA AJABU KWA SAUTI ZA UPINZANI:

Kufa kwa Magufuli hakukutokea tu kwa sababu alistahili kufa. Lakini ilikuwa lazima afe ili haya yatokee. Mwendazake Magufuli aliandaa na kutengeneza upinzani na huu ndiyo kisu kibaya. Huyu mama hawezi kukabiliana na wimbi la kelele hizi za mabadiliko na akabaki salama bila yeye kuanguka anguko kuu.

Wasichofahamu CCM ni kuwa upinzani huu ni wa aina yake. Haujawahi kuwepo tangu mwaka 1992. Unaanzia ndani ya CCM yenyewe na kushika kasi huku nje. Utabiri wa Nyerere J. K miaka karibu 30 iliyopita unatimia mdogo mdogo.

Hili halikuja kwa bahati mbaya. Linakuja ili kusudi la mabadiliko ya kiutwala wa nchi litimie.

CCM INAWEZA KUCHELEWESHA KWA KITAMBO KIDOGO MWISHO WAKE:

Nawashangaa ni kwanini wanapingana na kelele za harakati za mabadiliko ya katiba ya JMT ya 1977. Kwa hili, hawa ndugu zetu mtu aweza kusema bila shaka yoyote kuwa hawana akili, busara wala maarifa

Ndo kusema kuwa, wanaweza kulainisha wimbi la kelele za madai ya KATIBA MPYA YA WANANCHI kwa kukubali kwanza kufanya amendments kadhaa ili ku accommodate baadhi ya sensitive issues kulingana na mahitaji ya nyakati na majira.

Kushupaza shingo na kujaribu ku - opt "violence means" ili kuzima sauti hizi za kudai mabadiliko ya kiuongozi na utawala wa nchi hii, ni ku - speed anguko lao na bado wanalolikataa sasa likafanyika wakiwa nje.

Bado wako ndani. Watumie kikamilifu kanuni ya GIVE and TAKE. Wakubali kubaki na kidogo na pia kupoteza kidogo. Kama wanataka yawe yao yote, wakae tayari kupoteza yote.
 
Umezungumzia mengi ila hilo la mzanzibar kuitawala Tanganyika ni fikirishi zaidi, najua huwa wanampachika mzanzibar kwenye nafasi ya VP kama kielelezo cha kudumisha huu muungano, lakini kwa nini na kule Zanzibar asiwepo mtanganyika kwenye moja ya nafasi za juu serikalini ili kudumisha huo muungano?

Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania JPM, kinaweza kuwaamsha CCM next time waone kumbe inawezekana "kumpachika" kwao mzanzibar kama VP ipo siku anaweza akaja kuwa Rais accidentally bila wao kujiandaa na kusababisha misuguano ndani ya chama chao, kama wana akili watajifunza kwenye hili, na zaidi ukizingatia tofauti kubwa ya population iliyopo kati yetu na Znz.
 
Mh sawa nimeona ila niwachache wenye jicho la tatu kama wewe, atatokea rais ambae atatawala nusu wakati nae atatoweka juu ya uso wa dunia, nae alie chini yake atatawala hadi mwisho wa wakati baada ya hapo nchi itaamua vinginevyo, nao walio madarakani hawataamini macho yao maana ndani ya muda mfupi nchi itahama toka mikononi mwao.
 
Umezungumzia mengi ila hilo la mzanzibar kuitawala Tanganyika ni fikirishi zaidi, najua huwa wanampachika mzanzibar kwenye nafasi ya VP kama kielelezo cha kudumisha huu muungano, lakini kwa nini na kule Zanzibar asiwepo mtanganyika kwenye moja ya nafasi za juu serikalini ili kudumisha huo muungano?

Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania JPM, kinaweza kuwaamsha CCM next time waone kumbe inawezekana "kumpachika" kwao mzanzibar kama VP ipo siku anaweza akaja kuwa Rais accidentally bila wao kujiandaa na kusababisha misuguano ndani ya chama chao, kama wana akili watajifunza kwenye hili, na zaidi ukizingatia tofauti kubwa ya population iliyopo kati yetu na Znz.

Halileti maana...

Mpaka watoto wadogo wanauliza hili swali, la Mzanzibari kuwa Rais ktk nchi nyingine...

Nakuambia jambo moja, kuwa, ndani ya CCM yenyewe hili halukubaliki na ndilo lilosababisha "struggle for power" ndani ya CCM na ndani ya "system" ya nani awe Rais wa JMT kuchukua nafasi ya Mwendazake...

Inashangaza sana kuona CCM hawaioni kasoro hii na kwa makusudi au kwa ujinga tu wanapuuza kelele za mabadiliko ya katiba...!
 
CCM haiwezi kuanguka kirahisi hivyo, Hilo sahau kabisa. Tena sahau sana.

CCM ni mfumo wa utawala wa nchi. CCM sio tu ni chama bali ni nchi pia. Hili kila siku kumbuka nakuomba sana.

Ki deal na CCM hakuhitajiki akili ndogo namna hv, bali akili kubwa mno.

CCM sio wepesi hivyo. Na hv sasa ndo tupo kwenye harakati za kudai reform ya chama ndo kabisa, wapinzani watapoteana mazima
 
kama shetani alianguka itakuwa ccm? Uongo haujawahi kuushinda ukweli hata mara moja!
 
CCM haiwezi kuanguka kirahisi hivyo, Hilo sahau kabisa. Tena sahau sana.

CCM ni mfumo wa utawala wa nchi. CCM sio tu ni chama bali ni nchi pia. Hili kila siku kumbuka nakuomba sana.

Ki deal na CCM hakuhitajiki akili ndogo namna hv, bali akili kubwa mno.

CCM sio wepesi hivyo. Na hv sasa ndo tupo kwenye harakati za kudai reform ya chama ndo kabisa, wapinzani watapoteana mazima
Majira na nyakati yakifika, hakuna kinashindikana.

Goliath yule Mfilisti alikuwa na tambo kubwa na mbaya kuliko hili. Hakutumia akili na maarifa kutamba.

Aliangushwa na kuuwawa na mtu mdogo sana, aliyedharaulika.

Goliath CCM jiangalieni. Tumieni akili kuchelewesha kwa kitambo kidogo kifo chenu. Mnayo nafasi. Na sababu mnayo. Fanyeni ya hekima na busara.
 
Nikueleweshe , CCM ni chama makini. Kilichotokea 17.3.2021 hata viongozi in ndani ya chama hawajaewa Hadi Leo.pili katiba ya 1977 imekuwa kitanzi Kwa CCM

Kwenye nafasi ya urais. Iwapo chama kitatoa fomu za kutosha Kwa wagombea Urais,ni wazi kuwa mama ataangukia pua.
 
Halileti maana...

Mpaka watoto wadogo wanauliza hili swali, la Mzanzibari kuwa Rais ktk nchi nyingine...

Nakuambia jambo moja, kuwa, ndani ya CCM yenyewe hili halukubaliki na ndilo lilosababisha "struggle for power" ndani ya CCM na ndani ya "system" ya nani awe Rais wa JMT kuchukua nafasi ya Mwendazake...

Inashangaza sana kuona CCM hawaioni kasoro hii na kwa makusudi au kwa ujinga tu wanapuuza kelele za mabadiliko ya katiba...!
Hata sasa hivi ukiangalia kwa jicho la kawaida tu utaona kuna watu wako ndani ya CCM, na hata bungeni kwa shingo upande, siku hawa wakipata nguvu ya kuwarudisha juu hawatasita kufanya hivyo, japo kwa sasa litaendelea vuguvugu la chini, na hili litaendelea kuwatafuna CCM ndani kwa ndani mpaka uchaguzi mkuu ujao utakapowadia.
 
Suluhisho ni majimbo mawili ya kiutawala ya Tanganyika na Zanzibar chini ya Rais mmoja wa Jamuhuri.Kila jimbo linakuwa na waziri mkuu wake au Gavana, bunge lake lenyewe, mfumo wa mahakama zake na mahakama kuu za Rufaa na Katiba za kitaifa.
Umezungumzia mengi ila hilo la mzanzibar kuitawala Tanganyika ni fikirishi zaidi, najua huwa wanampachika mzanzibar kwenye nafasi ya VP kama kielelezo cha kudumisha huu muungano, lakini kwa nini na kule Zanzibar asiwepo mtanganyika kwenye moja ya nafasi za juu serikalini ili kudumisha huo muungano?

Kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania JPM, kinaweza kuwaamsha CCM next time waone kumbe inawezekana "kumpachika" kwao mzanzibar kama VP ipo siku anaweza akaja kuwa Rais accidentally bila wao kujiandaa na kusababisha misuguano ndani ya chama chao, kama wana akili watajifunza kwenye hili, na zaidi ukizingatia tofauti kubwa ya population iliyopo kati yetu na Znz.
 
CCM haiwezi kuanguka kirahisi hivyo, Hilo sahau kabisa. Tena sahau sana.

CCM ni mfumo wa utawala wa nchi. CCM sio tu ni chama bali ni nchi pia. Hili kila siku kumbuka nakuomba sana.

Ki deal na CCM hakuhitajiki akili ndogo namna hv, bali akili kubwa mno.

CCM sio wepesi hivyo. Na hv sasa ndo tupo kwenye harakati za kudai reform ya chama ndo kabisa, wapinzani watapoteana mazima
Mambo yanayotokea kwa sasa ni kama yanaacha nyufa kwenye kuta za nyumba ya CCM, mtaendelea kutafunana taratibu ndani kwa ndani, siku ikifika ikawepo na nguvu toka nje, nyie ndio mmekwisha mazima, nakumbuka hata wewe ulijiita CCM msomi unaetaka Katiba Mpya, najua wa aina yako mnapigwa vita sana ndani ya chama chenu, wacha hiyo vita iendelee..
 
Suluhisho ni majimbo mawili ya kiutawala ya Tanganyika na Zanzibar chini ya Rais mmoja wa Jamuhuri.Kila jimbo linakuwa na waziri mkuu wake au Gavana, bunge lake lenyewe, mfumo wa mahakama zake na mahakama kuu za Rufaa na Katiba za kitaifa.
Haya maoni yako yanafanana na ile rasimu ya Warioba kama sijakosea.
 
Tungekuwa na upinzani makini hayo unayofikiria labda yangewezekana. Lakini kwa bahati mbaya hatuna chama cha upinzani wala mpinzani wa kweli.

Sabodo alimkabidhi mwenyekiti wa chadema mamilioni ya shilingi ili ajenge ofisi za chama na kuchimba visima katika maeneo mbali mbali ya nchi, kwa lengo la kuwavuta watu wajiunge na chama lakini matokeo yake mwenyekiti akatumia mamilioni yale kwenda kula bata na wema sepetu dubai, na aliporudi kutokana na nguvu alizonazo ndan ya chama hakuna mtu aliefungua kinywa chake kumuuliza chochote kuhusiana na mamilioni aliyotafuna.

Kama hiyo haitoshi mwenyekiti na genge lake wakaja na plan ya kuwachangisha wabunge kila mwezi. Wabunge wakachangia chama kwa kipindi cha miaka mitano lkn mpaka leo hawajui hela hizo zimekwenda wapi na hapo hatujazungumzia ruzuku ya chama iliyokuwa inapokea wakati wa utawala wa Kikwete na Magufuli, hela za michango wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, bado misaada ya mamilioni kutoka kwa wafadhili wa chama kule ulaya.

Zote hizi zinatafunwa na mwenyekiti pamoj na genge lake la kumtetea hapa mitandaoni ili kufunika mabaya yake na ya chama kwa ujumla. Lipumba, Zito na Mbatia hawa ndo tunawatumia tutakavyo kudhoofisha upinzani nchini. Kifupi hakuna upinzani wa kuitoa CCM madarakan labda miaka 40 ijayo. Baada ya hawa wenyeviti wachumia matumbo kustaafu siasa au kutoka kweny nafasi zao.
 
Back
Top Bottom