Tungekuwa na upinzani makini hayo unayofikiria labda yangewezekana. Lakini kwa bahati mbaya hatuna chama cha upinzani wala mpinzani wa kweli. Sabodo alimkabidhi mwenyekiti wa chadema mamilioni ya shilingi ili ajenge ofisi za chama na kuchimba visima katika maeneo mbali mbali ya nchi, kwa lengo la kuwavuta watu wajiunge na chama lakini matokeo yake mwenyekiti akatumia mamilioni yale kwenda kula bata na wema sepetu dubai, na aliporudi kutokana na nguvu alizonazo ndan ya chama hakuna mtu aliefungua kinywa chake kumuuliza chochote kuhusiana na mamilioni aliyotafuna. Kama hiyo haitoshi mwenyekiti na genge lake wakaja na plan ya kuwachangisha wabunge kila mwezi. Wabunge wakachangia chama kwa kipindi cha miaka mitano lkn mpaka leo hawajui hela hizo zimekwenda wapi na hapo hatujazungumzia ruzuku ya chama iliyokuwa inapokea wakati wa utawala wa Kikwete na magufuli, hela za michango wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, bado misaada ya mamilioni kutoka kwa wafadhili wa chama kule ulaya. Zote hizi zinatafunwa na mwenyekiti pamoj na genge lake la kumtetea hapa mitandaoni ili kufunika mabaya yake na ya chama kwa ujumla. Lipumba, Zito na Mbatia hawa ndo tunawatumia tutakavyo kudhoofisha upinzani nchini. Kifupi hakuna upinzani wa kuitoa CCM madarakan labda miaka 40 ijayo. Baada ya hawa wenyeviti wachumia matumbo kustaafu siasa au kutoka kweny nafasi zao.