Mama Anacheza game kwa umakini sana,anajua hawezi Watema MATAGA kwa sasa,anawahitaji kupanga safu yake,along the way,mchele na pumba utajitenga tu
Hata hawa activists wa mitandaoni ameanza nao vizuri,full kuwapiga chenga,Kuna msemo mmoja niliusikia Aliutoa Jk Juzi Kati kwenye mazishi naona ndio unafanya kazi sasa,MSICHEZE NGOMA YA ADUI,Mpaka Msigwa kapigwa chenga Jana.
Kwa kifupi Ana washauri wazuri,teuzi zilizofanyika sasa ni kujitoa lawama,ila anajua alichofanya,ndio maana mwisho Alitoa angalizo..
Report ya TAKUKURU Ikitoka,itabeba wengine,anakutoa ofisini kwa ushahidi,inaonekana anaanza kuzipa taasisi meno kama ataendelea hivi
Itamlazimu,nasema tena,Itamlazimu Kuheshimu KATIBA Sababu namna ya alivyopata Urais wake kuna watu Wamesimamia na kuheshimu Misingi hiyo ya KATIBA,Pasi na Shaka hili ni deni Kubwa sana alilonalo..
KERO ZA MUUNGANO Ameishaanza kuzivalia njuga Kabla hata hajaanza,Ni mzanzibari,kwa teuzi alizofanya tutegemee mabadiliko mengi kwenye muungano,rejea Maagizo aliyotoa kwa Waziri wa fedha..
Kwa kifupi huyu Mama KATIBA ataitendea haki,kwa mawazo yangu,ni kitu kiko kichwani mwake kabisa,rejea slip tongue aliyoifanya jana katika teuzi za Baraza la mawaziri..
Niwatakie siku njema...