Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,895
- 20,392
Wadau, amani iwe kwenu.
Katika historia ya upinzani nchini, mwaka 2015 ulikuwa ni uchaguzi ambao ulitushughulisha sana wana CCM. Hata hapa kwenye jukwaa mijadala ilikuwa ni mikali na mnyukano kati ya CCM na CHADEMA ulikuwa wa wazi.
Nakumbuka wakati huo ukianzisha mjadala wa kumshambukia kiongozi wa CCM ama upinzani thread ilikuwa inatembea sana.
Hali ya kisiasa wakati huo ilibebwa na uamuzi wa Lowasa kuhamia CHADEMA. Ni kwa mazingira hayo hata sisi ndani ya CCM tuligawanyika na ndo maana upinzani ulipata nguvu.
Binafsi nilikuwa ni wafia chama hasa wa kambi ya CCM. Nikawa natumia nondo nilizokuwa nazo kumgonga hasa Lowasa. Nilifanikiwa kupata mikakati yake mingi na kuiumbua kabla haijafanikiwa. Aisee nilitisha sana wakati ule.
Baada ya CCM kuibuka ushindi katika uchaguzi ule, binafsi niliona nimeshamaliza kazi na nikaamua kuja hapa Uingereza kujiendeleza kimasomo na kula bata.
Uchaguzi wa 2020 haukuwa na upinzani kabisa isipokuwa CHADEMA walibebwa na tukio la Lissu kupigwa risasi ambalo wao wenyewe ndio walilitengeneza kwa maslahi yao ya kisiasa. Bahati mbaya sana mtaji huo haukuwalipa na CCM tukashinda kwa kimbunga.
Uchaguzi wa 2025 nauona ukiwa wa upande mmoja kwa asilimia 95. Mtaji wa risasi za Lissu haupo tena na CHADEMA hawana agenda za kuwaambia wananchi. Kila wanalofikiria mama keshatangulia kitambo. Si mmewaona juzi kwenye mkutano wao wa hadhara! Wamebaki kuisifi CCM na Rais mama Samia. Kawazidi kete. Kwa sasa watajitutumua kiasi ila kampeni za 2025 mtaona zitakavyododa kwa upande wao.
Hongera sana Mheshimia Mama Samia. CHADEMA mwendo wameumaliza