PostGE2025 Rais Samia Suluhu Hassan ametimiza Mwaka moja tangu aapishwe Novemba 3, 2025

PostGE2025 Rais Samia Suluhu Hassan ametimiza Mwaka moja tangu aapishwe Novemba 3, 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametimiza mwaka mmoja tangu kuapishwa kuiongoza nchi kwa muhula mpya, kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Rais samia Alipata ushindi wa kura 31,913,866 sawa na asilimia 97.66 ya kura zilizopigwa dhidi ya wagombea 16 wa vyama vingine.

Maadhimisho hayo yanatoa nafasi ya kutazama kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake, ikiwemo hatua zilizochukuliwa na Serikali katika masuala ya uchumi, maendeleo ya jamii, huduma za kijamii na utekelezaji wa ahadi za kisera.

Hata hivyo, kipindi hicho kimekuwa na mijadala mbalimbali kuhusu mwenendo wa kisiasa na kijamii nchini, hususan masuala ya demokrasia, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na matukio ya vurugu yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Rais Samia aliapishwa Novemba 3, 2025, katika hafla iliyofanyika Chamwino, Dodoma, baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu.

Mwaka mmoja wa muhula huo mpya unatoa fursa ya kutathmini utekelezaji wa ahadi za Serikali, mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza na matarajio ya wananchi katika kipindi kilichobaki cha uongozi wake
 
Kupata futuhi kama hizi tubonyeze ngapi bwashee?
 
Sio mbaya. Amebakiwa na miezi 48, au siku 1,461, au masaa 35,064 ya utawala wake. Watanzania tuwe wapole na tumpe ushirikiano amalizie angu yake ya pili.
 
Acheni kumtia ujinga. Urais aupate wapi? Nani wa kumchagua huyu mzanzibar? Kapachikwa tu na mafisasu wa Nchi hii sababu wanajua hana uelewa wa utawala ili waibe bila kusumbuliwa.

Ndo maana muda wote amejificha sababu anajua hajachaguliwa.

Magufuli alikuwa anatembelea Magomeni, Kariakoo, Kigamboni, Feri anakunywa kahawa na wapiga debe. Hata yeye anajua hqjqchaguliwa ndo maana muda wote kajifungia Kizimkazi. Na 2030 kwake ni mbali sana.
 
Back
Top Bottom