KUHUSU KUTUMIA NGUVU NYINGI KULIKO AKILI KWENYE ULIZI WA MADNI
Mirerani tumejenga ukuta, kuta la kwelikweli tukaweka na Majeshi lakini Madini yanatoroshwa kama mwanzo, tukibahatika kuliona linaoneshwa hili hapa, piga picha, bonge la Tanzanite, tunajua mabonge mangapi yamepitishwa chini kwa chini yakatoka?, hatujui”———Rais Samia
“Ndani ya Mirerani kuna vitaru, kitaru C kimewekwa akiba lakini sasa kimeanza kuvamiwa, nataka niseme sitaki kuona mkono wa Mtu kwenye kitalu C, walioanza kugawa vitaru kwenye hilo eneo acheni kina matumizi yake”———Rais Samia
KUHUSU WAWEKEZAJI KUMNYWA
“Wawekezaji wanalalamika sana kumekuwa na urasimu mkubwa Tanzania, kodi kwa Wawekezaji hazieleweki, napokea taarifa kutoka kwa Wasaidizi wangu, Wafanyabiashara wanataka kuniona niwahakikishie kama watafanya kazi kwa utulivu ili warudi Tanzania”——-Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo
“Wawekezaji wanataka kuja Tanzania lakini kwa mambo yetu wanakimbia, tuvute tena uwekezaji, tupate ajira,fedha izunguke,uchumi ukue, nikiwa Makamu wa Rais kuna Mwekezaji alikuja, sijui alitishwa nini!, nadhani kaambiwa tutakupiga kosa la uhujumi uchumi, akaondoka”———Rais Samia
“Vibali vya kazi vimekuwa janga, wanaosimamia vibali vya kazi wamejigeuza Miungu Watu , wamegeuza mradi, Mtu anawekeza mnalazimisha aweke Mtanzania, kila Mwekezaji ana haki ya kuweka Mtu anayemuamini yeye kwanini umlazimishe?, mtende haki”———Rais Samia
“Tunataka Wawekezaji wa-enjoy Tanzania, Makampuni yanafungwa Ndugu zangu sio uongo, tukiweka vikwazo tunawarudisha nyuma, wakiondoka uchumi wetu unashuka, ajira zinapungua na mzunguko wa pesa unapungua na hiki ndio kilio kikubwa cha Watanzania kuwa mifuko mitupu”———Rais Samia
#MillardAyoIkuluUPDATES
CORONA
Tutaunda Kamati ya Wataalamu kuhusu Covid 19 watuambie kitaalamu hayo yanayopendekezwa na Ulimwengu kuja kwetu yapoje, hatuwezi kujitenga tu kama Kisiwa na hatuwezi kupokea yanayoletwa bila kuweka cha kwetu, bila kufanya utafiti wa kwetu”———Rais Samia
“Rais Kikwete alituambia akili za kuambiwa changanya na zako, tuweke na zetu tuwe na msimamo maalum unaoeleweka, sio tunasoma tu mambo ya Covid 19 Ulimwenguni, Tanzania deshi deshi deshi haieleweki, tueleweke kama tunakubali au tunakataa”———Rais Samia
TRA KUTUMIA VITISHO NA MABAVU KUKUSANYA KODI
“TRA agizo langu kwenu ni kuacha matumizi ya ubabe na mabavu kwenye kukusanya kodi haisaidii, mtakwenda mtambinya Mtu, mtamkamua, mtamtisha na kupiga uhujumu uchumi anaogopa kwenda Jela atajikwangua atalipa lakini unaua biashara anafunga, kesho nani anakulipa kodi?”——-Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi wapya Ikulu Dar es salaam leo
UHURU WA KUTOA MAONI BILA HOFU YA KUMNYWA
“Wizara ya Habari, nasikia kuna Vyombo vya Habari mmevifungia, sijui Viji- TV vya mikononi vile, vifungulieni lakini wafuate sheria na miongozo ya Serikali, tusiwape mdomo wa kusema tunabinya Uhuru wa Vyombo vya Habari, tusifungie tu kibabe”———Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi Wapya leo Ikulu Dar es salaam
MABANDO
“Kuhusu suala la mabando kulizuka rabsharabsha juzi hapa, Wananchi wakapiga kelele mkalituliza, kalifanyieni kazi lisizuke namna ile mpo mnaangalia hawa Watu wanakuja tu na mambo yao mpaka Wananchi washtuke na nyie ndio mnashtuka, kakaeni nao”———Rais Samia Suluhu baada ya kuwaapisha Viongozi Ikulu Dar es salaam leo
View attachment 1745356