Rais Samia Suluhu Hassan: Kwenye nchi zetu mbili moja ina 'uhuru' wa kufanya biashara na nyingine ina 'suluhu' ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara

Rais Samia Suluhu Hassan: Kwenye nchi zetu mbili moja ina 'uhuru' wa kufanya biashara na nyingine ina 'suluhu' ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara

Behaviourist

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2016
Posts
39,926
Reaction score
95,626
Haya ni maneno ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara yake huko Kenya.Haya maneno yamenishtua sana na kunifanya nijiulize maswali lukuki.

Ni nani huyo mtu ambae aliweka vikwazo vya Kufanya biashara Tanzania hadi ihitajike 'Suluhu'? Wananchi wa Tanzania walimchukulia hatua gani mtu huyu?Alipata wapi nguvu na ujasiri wa kufanya yote haya?Sheria za Tanzania pamoja na utamaduni wa Tanzania viliruhusu vipi mtu huyo kufanya ujinga wote huu?


 
Kinachofanyika kwa Sasa ni kuua Neo colonialism,kabla ya berlin conference mahala ambapo matatizo yote yalianza hizi nchi zote Hadi kurudi nyuma ziliishi in harmony, wacha turudishe Zama zetu za kale Kama kawaida.

Hongera Sana Mama SSH na Uhuru akili zenu ni sawa kwa raia wa pande zote mbili, mwenye akili na apambane siyo kubwabwaja.
 
We unaakili ya kukalia keyboard tu, ametaja majina ya maraisi kumalizia hotuba.
Naam nafikiri hivi hata Mimi, amependa
Katumia majina ya suluhu na uhuru kigezo cha kwanza,

Maana halisi ni juu yako wewe msomaji,
Hawezi kulimit fikra na mtazamo wako
 
Naam nafikiri hivi hata Mimi, amependa
Katumia majina ya suluhu na uhuru kigezo cha kwanza,

Maana halisi ni juu yako wewe msomaji,
Hawezi kulimit fikra na mtazamo wako
Mwwndazake aliwahi kuchomekea majina ya marais wa nchi mbili kati ya Tz na Zambia

"Huku kuna Pombe na huko kuna Lungu, si mnajua mtu akinywa pombe huku ameshika lungu inakuaje"

Tumeona matokeo yake
 
We endelea kucheka na hao WAKENYA ukidhani ndugu zako.
Mama nahisi hawajui vizuri manyang'au, wale jamaa wanaangalia watabenefit vipi tu, kwa huu uhuru na suluhu anayoitaka mama tz ndio tunaenda kuwa looser
 
Mama anaturudishia nchi yetu yenye maziwa na awali, mama apongezwe kwa hilo, wasio mpenda wasage chips wameze

Tupo pamoja na mama, haijalishi wewe chama gani Tanzania Kwanza.
 
Mama nahisi hawajui vizuri manyang'au, wale jamaa wanaangalia watabenefit vipi tu, kwa huu uhuru na suluhu anayoitaka mama tz ndio tunaenda kuwa looser
Rostam alitoa statistic data kabisa kuonyesha jinsi gani hawajamaa wanavyojua kutuchezea
 
Back
Top Bottom