Mtukudzi
Senior Member
- Nov 14, 2013
- 104
- 413
Naungana na watanzania kumpa pole kiongozi wetu Mh. Rais Suluhu kwa msiba wa Hayati Dr. Magufuli. Apumzike kwa amani.
Tanzania ni nchi yetu sote na hatuna 'nchi mjomba'. Kwa hiyo tuipende nchi yetu. Serikali iliyopo madarakani inaweza isipendwe lakini siyo nchi.
Baada ya utawala wa awamu ya tano kuingia tulianza kuona watumishi wengi wakiacha kazi hapa nchini na kupeleka ujuzi wao nje ya nchi na wengine kuacha taaluma zao na kufanya mambo mengine. Hali hii ilisababisha kuwepo upungufu mkubwa wa watumishi karibu kila kada katika utumishi wa umma.
Hali hii imepelekea kushuka kwa morali kwa wafanyakazi wachache waliobaki kwa sababu workload ni kubwa na incentives hakuna.
Mfano halisi utauona kwenye miradi ya TAMISEMI inayotekelezwa kwa FORCE ACCOUNT. Miradi hii asilimia kubwa haijakamilika. Wanachofanya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa(MSM) ni kupiga rangi kwa nje na kutuma picha kwa katibu mkuu kuwa mradi upo 95% kwa WOGA wa kutumbuliwa !
Kiuhalisia miradi mingi haijamilika ili kuweza kutoa huduma. Kuthibitisha hilo waulize wale madaktari walioenda kuanzisha Hospitali mpya za Wilaya na vituo vya afya nchini. Miradi hii utekelezaji wake ulifanywa na LOCAL fundi kwa kusimamiwa na maafisa MAENDELEO ya JAMII kama wahandisi. Wahandisi wengi wameacha kazi.
Ukienda kwenye kada ya madaktari na sekta ya afya utakuta watumishi wengi wameondoka makazini na shift zinakuwa ngumu sana kwa waliobaki.
Hali hii iko kwenye kada na maeneo mengi ya utumishi kwa sasa.
Natambua ni gharama sana kuajiri mtumishi mpya na kuacha yule ambaye tayari ameishakuwa mzoefu kazini. Ndiyo maana Rais Kikwete alifanikiwa kuleta nchini Watanzania waliokuwa wanafanya kazi nzuri huko nje japokuwa baadae walikuja kujilaumu baada ya JK kuondoka.
Nashauri mh. Rais awaombe kurudi kazini watumishi ambao waliondoka kazini baada ya kuwa mistreated na kuamua kuacha kazi. Watu hao wengi bado wako kwenye payroll japokuwa hawapokei mishahara kwenye account zao. Kigezo kikubwa iwe ni watumishi amabao hawakuwahi kuwa na matatizo ya maadili katika utumishi wao.
Hii itaisaidia serikali dhidi ya wimbi jipya la watumishi kutaka kustaafu kwa hiari baada ya kufikisha miaka 55 hali inayoelemea mifuko ya hifadhi za jamii.