Rais Samia Suluhu Hassan, sambaratisha Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu

Fedha za kugharamia Kurugenzi hii zielekezwe kwenye matumizi mengine. Nawasilisha!
Tatizo letu watanzania kila mtu ni mjuzi
Hujawahi hata kufika geti la ikulu lakini unashauri kitengo kivunjwe.
Rais anatakiwa awe na mwandishi wake wa habari popote alipo hata kama ni msibani
Rais anatakiwa awe na wapiga picha wake,haiwezekani kuwa na mmoja,lazima wawe wawili na kuendelea kwa ajili ya shift na kupokezana kazi
Kunatakiwa kuwe na mtu wa mitandao ya jamii n.k
Kitengo cha habari ikulu kinatakiwa kutoa habari zote za Rais na ikulu kwa ujumla,msidhani watu wanakula raha kule
 
Soma uzi kwa utulivu hutoumia ubongo. Nani kakukatalia hao uliowataja hawapo? Ikulu ni nyumbani kwangu!
 
Gazeti la Mtanzania?
Salva hajawahi kumiliki gazeti. Mtanzania, Rai, Dimba na The African chini ya New Habari Cooperation ni Mali ya Rostam Aziz. Huko nyuma kampuni ikiitwa Habari Cooperation ilimilikiwa na Jenerali Ulimwengu kabla ya kuuza kampuni hiyo na kuanzisha Raia Mwema. Salva alikuwa Mhariri na Mchambuzi.
 
Hivi kwa nchi ambayo tayari tumeshafikia uchumi wa kati, tunatengenezaje ajira kwa watu wetu wasiokuwa na ajira? Hiki kitu mimi nakiona ni kama mojawapo sasa ya fursa za ajira zilizojitokeza baada ya mambo yetu kuwa yamekuwa mazuri, pamoja na kwamba kilianza kabla hatujafikia uchumi wa kati.

Mimi nashauri tusiwe wabahili sana, tutawaumiza wengine ambao nao pia wanayo nafasi ya kufurahia fursa za ajira ndani ya serikali
 
Nawasalimu Kwa Jina La
Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
💋👄💋💘👄👄💋💋💋💘💘😘
Ninyi Sasa Mtajibu
Kazi Iendelee!!😁😀
 
hakuna mshahara wala posho ya milioni 15 kwa siku , tatizo lako labda unataka Msigwa aondoke ikulu kwakua ana vyeo viwili thats it , lakini uzi haujakaa kama unavyotaka uwe, ufisadi haupo ila ni vyeo tu mkuu
 
Hicho kitengo ni upigaji tu wa pesa za walipa kodi. Kazi kubwa ya Msigwa ni kuweka barua za uteuzi na utenguzi Twitter.Huhitaji kurugenzi kwa hiyo kazi. Mtu mmoja tu anatosha.

Kingekuwa na mantiki na umuhimu kama Msigwa angekuwa anafanya mikutano ya mara kwa mara, hata mara moja kwa mwezi kuwapa waandishi wa habari fursa ya kuuliza mambo mbalimbali yanaoendelea katika ofisi ya Rais

Kingekuwa na mantiki pia kama Marais wetu wangekuwa na utaratibu wa kuzungumza na waandishi wa habari kiwe kinaratibu hiyo mikutano.
 
Naunga mkono hoja. Mama apewe muda na sapoti ajipange. Mpaka sasa anakwenda vizuri
 
Ifanye kazi za kurugenzi sasa. Iwe inaita waandishi wa habari waulize mambo yanayohus ofisi ya Rais sio kutuwekea barua za teuzi na tenguzi tu
Hii kurugenzi iendelee hata kama ilianzishwa kimagumashi kumpa ulaji salva
 
Shida yako ulitaka kusema kuhusu corona au ghalama za hiyo kurugenzi?

Abas kasema kuhusu mengi sasa wewe umeona kusemea corona tu ndo hasara ya hiyo kurugenzi au ulitaka kuzungumzia corona?

Ukiona hilo ni shida basi kila kitu ikulu kifutwe ili Raisi abaki na walinzi tu hata kula atakula kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…