Abraham Moshi
Member
- Jan 16, 2012
- 20
- 8
Ni kuhusu maelekezo yaliyotoka Serikalini tarehe 08 Februari,2021 kuidhinishwa Muundo mpya wa maendeleo ya Utumishi (Scheme of Service) Ulioanza kutumika terehe 01 Machi 2021) kwa baadhi ya taasisi za Umma.
Kutokana na mabadiliko ya Muundo huo imeonekana kuwa, Mishahara ya watumishi hao ni mikubwa kuliko mishahara iliyopo katika Muundo mpya wa watumishi wa umma.
Ili waendelee kulipwa mishahara hiyo wanayolipwa sasa, Wakuu wa baadhi ya taasisi za Umma waliamua kuwaombea kibali cha mishahara binafsi Serikalini watumishi hao watakao athilika na muundo huo mpya.
Aidha kulingana na Muundo huo mpya Madaraja ya viwango vya mishahara yalipunguzwa kutoka ngazi 9 hadi kufikia ngazi 5 pia vyeo vya watumishi hao vilibadilishwa ili kuendana na Muundo huo kandamizi usio na tija.
Athari zinazotokana na Muundo huu, wafanyakazi ambao wapo katika kundi hili hawataweza kupanda vyeo tena (Promotion), wala nyongeza ya mshahara, Jambo hili limewaathiri sana kisaikolojia.
Tunaomba ufumbuzi wa jambo hili haki itendeke kwa maslahi ya watumishi wa umma na Taifa kwa ujumla, kwa kuwa watumishi hao wengi wao ni waajiriwa wa chini ya mwaka 2004 walipanda madaraja yao kihalali tokana na juhudi zao na utumishi wao wa muda mrefu hadi walipofikia sasa.
Jambo la kushangaza na kusikitisha iweje watumishi hao wahukumiwe na mabadiliko ya Muundo mpya unao sababisha wapoteze haki zao za msingi za kupanda vyeo na nyongeza za mishahara? Tunaomba Muundo mpya uzingatie haki za watumishi hao waliolitumikia Taifa hili kwa muda mrefu na kwa uadilifu mkubwa.