Rais Samia Suluhu kamwe usirithi maadui, tengeneza wa kwako

Rais Samia Suluhu kamwe usirithi maadui, tengeneza wa kwako

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Ningelipata nafasi ya kuonana na rais SSH ningelimuuma sikio na kumpa tahadhari kwamba awe kama ndege mbayuwayu (akili za kuambiwa achanganye na zake.

Rais SSH bado ana kundi kibwa Sana la watu ktk serikali yake waliokuwa wameaminiwa na mwendazake. Na kimsingi watu hawa walijipanga kufaidi mema ya nchi hii hata baada ya 2025. Lkn ghafla ndoto zao zimekatizwa kufuatia kifo cha ghafla cha godfather wao.

Mama alipoingia akawaondoa kwenye viti vyao na magari yao ya kifahari. Na wengine wamebadilishiwa nafasi i.e wameondolewa mahala penye ulaji na kupelekea mahala kwenye uhitaji wa mitaji. Sonono zimewajaa mioyoni japo usoni wanacheka.

Wanaumiza vichwa na kujiuliza watarudi vipi ktk nafasi zao za kula kuku kwa mrija??? Hapa ndipo wanatengeneza mitego maalumu ya kuudhoofisha utawala wa mama bila ya mama mwenyewe kujua. Wanampa ushauri wenye kumnasa huko mbeleni.

Mama amepewa ushauri wa kuendelea na maadui wa awamu ya tano na ameupokea. Lkn sidhani kama atakuwa na nguvu ya kuhimili mikikimikiki ya maadui hawa huku akiwatumikia watanzania kwa ufanisi.

Ili kuhimili anapaswa kuwa na roho mbaya ya kuuwa, kuteka, kujeruhi kwa risasi, kupora watu na kudukua mazungumzo ya wanaomteta. Sioni kama mama ana roho yenye uovu wa kiwango hiki. Na kama kweli hana basi, hakupaswa kufuata njia ya mwendazake ktk kuongoza nchi.

Hawa wafuasi wa mwendazake furaha yao itatimia pale ambapo wananchi wote, Jumuiya za kimataifa na nchi wahisani watakapoimba wimbo mmoja ...."mama hafai". Ikifikia hapa jeshi litachukuwa nchi na kuikabidhi kwa waliosuka mission. Utawala wa awamu ya sita utakuwa umeishia hapo na wafuasi wa mwendazake watakula na kunywa kishangilia ushindi.

Mama ajiangalie, asichukuwe kila ushauri. Anapaswa kuongoza nchi kwa staili yake. Na kamwe asirithishwe maadui.
 
Unajidanganya sana. Hivi tangu mkapa wamebadilika wangapi. Yeye Samia katoka wapi. Shida ya kupambana na Marehemu. Huwezi Shinda vita hiyo. Pumzika.
 
Unajidanganya sana. Hivi tangu mkapa wamebadilika wangapi. Yeye Samia katoka wapi. Shida ya kupambana na Marehemu. Huwezi Shinda vita hiyo. Pumzika.
Marehemu kaacha mbegu mbaya. Acha tuendelee kuing'oa.
 
SSH ni CCM , kama mwenyekiti wa CCM adui wa CCM ni adui wake wa kurithi, mama watandike tu chama kinakutegemea🐒
 
SSH ni CCM , kama mwenyekiti wa CCM adui wa CCM ni adui wake wa kurithi, mama watandike tu chama kinakutegemea🐒
Unapotoa ushauri kumbuka kwamba Mdude ana wembe wa kumnyolea.
 
Mkuu wa mkoa wa mwanza kamuweka Samia katika wakati mgumu, bloody mess.
 
Mkuu wa mkoa wa mwanza kamuweka Samia katika wakati mgumu, bloody mess.
Huyu RC Sidhani kama amejiamulia kufanya hivi. Kwa vyovyote kapokea maagizo toka juu (kwa SSH mwenyewe)
 
Back
Top Bottom