Rais Samia Suluhu kumshukuru kwa ishara mhudumu wa Air Tanzania ni ishara ya Utumishi unaoheshimu wadogo na wakubwa

Rais Samia Suluhu kumshukuru kwa ishara mhudumu wa Air Tanzania ni ishara ya Utumishi unaoheshimu wadogo na wakubwa

Hivi haya mambo ya kusifia kila kitu nilidhani / nili-hope kwamba yatakuwa yamefikia kikomo....

Tusije tukarudi kule kule tulipotoka kwa watendaji badala ya kutenda wakawa wasifiaji
 
Wewe mama wa Kihaya una macho yanayoona mbali sana, imenibidi nitafte hii clip kuona unalolisema. True anaonekana akishukuru, Kwanza kitendo Cha kumwona huyu muhudumu wakati tumezoea viongozi wengi uelekeza macho kwa wenyeji wao ni ishara ya makuzi. Huu unaitwa uongozi unaoacha halama bila kutumia maneno. Hii video naidownload kiongozi akifoka namtag😂😂😂😂😂kumkumbusha zama za kufokafoka zimepita sisi sote ni binadamu tuna Hali yakuheshimiwa na tutaadhibiwa baada yakuthibitika tuna hatia
Halama ndio nini we jamaa
 
Usichokijua huyo muhudumu ni ofisa wa juu wa kitengo.wanajuana hao
 
We ulikula shingapi mwaka 2015, maana umekuwa msafishaji mkubwa wa madudu ya mwenyekiti hapa jukwaani. Hata hivyo tetea yako haisaidii kuwaingiza wapinzan ikulu daima.
Corona inaua
 
Usichokijua huyo muhudumu ni ofisa wa juu wa kitengo.wanajuana hao
Haitusaidii sisi tunacho kisifu ni utayari wa rais kujishusha kwa watanzania na siyo kufokafoka tuuu kama watu wa hi hop
 
Mbona kawaida marais wengi wanafanya hivyo Ila nawakubali Sana Trump Kuna siku alikuwa anaboard airforce one ( helcopter) Kuna mhudumu Askari alikuwa amekakamaa kwa saluti mlangoni upepo ulikuwa mkali kofia ya yule Askari ikapeperushwa na upepo ikaanguka , Trump aliinama akachukua ile kofia akamvalisha yule Askari halafu naye Trump akampigia saluti yule Askari.
Trump alikuwa very gentleman kwa watu wa chini
Nimetamani kuona hii clip,ni heshima kubwa sana
 
Wakati Mhe. Rais anaingia jijini Dar akitokea Dodoma ameonekana akitoa shukrani kwa muhudumu wa ndege Jambo ambalo viongozi wengi awafanyi kwa watumishi wa chini yao.

Viongozi wengi wanapopata madaraka wamekuwa watu wa dharau na kufoka kwa walio chini yao. Wengi wamekuwa watu wakuona mapungufu kwa wadogo na si mazuri.

Nikupongeze Mhe. Rais kwa ulichokifanya, najua ukujipanga kufanya hivyo ila umefanya kwa sababu ndivyo ulivyolelewa na kukuzwa. Ila baada yakufanya hivyo sisi wa chini yako na wananchi tumeitafsiri hii Kama ishara yakurudisha nidhamu na heshima ndani ya Utumishi na jamii kwa mkubwa kumheshimu mdogo kadhalika kwa mdogo kumheshimu mkubwa.

Umemtia moyo sana huyo muhudumu wa ndege lakini pia umewatia moyo wengi waliokuwa na hofu dhidi ya watu wenye madaraka.

Niwatake viongozi wengine mjifunze kuheshimu walinzi, wapishi, wafanyakazi wa ndani, wahudumu, wasaidizi na kila mtu unayeinteract naye katika maisha binafsi na maisha ya kazi. Tuache kujimwambafai tukiamini titaogopeka.

Respect my president.
Tunaomba video yake na sisi tuone maana yakuambiwa tuchanganye na yakwetu
 
Mbona kawaida marais wengi wanafanya hivyo Ila nawakubali Sana Trump Kuna siku alikuwa anaboard airforce one ( helcopter) Kuna mhudumu Askari alikuwa amekakamaa kwa saluti mlangoni upepo ulikuwa mkali kofia ya yule Askari ikapeperushwa na upepo ikaanguka , Trump aliinama akachukua ile kofia akamvalisha yule Askari halafu naye Trump akampigia saluti yule Askari.
Trump alikuwa very gentleman kwa watu wa chini
 
Haitusaidii sisi tunacho kisifu ni utayari wa rais kujishusha kwa watanzania na siyo kufokafoka tuuu kama watu wa hi hop
Hizo zote ni tabia za binadamu kwa akili yako fupi ulitegemea wafanane!!??
 
Tanzania ni yetu sote. Mpaka yule mzibua choo kisijae kikaleta kipindupindu ni shujaa wa nchi.
 
Huyu Mheshimiwa mpya enzi za jiwe atakuwa aliishi kwa shida sana,
 
Mbona kawaida marais wengi wanafanya hivyo Ila nawakubali Sana Trump Kuna siku alikuwa anaboard airforce one ( helcopter) Kuna mhudumu Askari alikuwa amekakamaa kwa saluti mlangoni upepo ulikuwa mkali kofia ya yule Askari ikapeperushwa na upepo ikaanguka , Trump aliinama akachukua ile kofia akamvalisha yule Askari halafu naye Trump akampigia saluti yule Askari.
Trump alikuwa very gentleman kwa watu wa chini
Nadhani ni protocol kujibu salute ndo chombo kondoke, refer hii ya Obama.

Back
Top Bottom