Rais Samia Suluhu tunaomba sana uturudishie biashara ya viumbe hai nje ya nchi

Rais Samia Suluhu tunaomba sana uturudishie biashara ya viumbe hai nje ya nchi

Chris wood

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2020
Posts
1,667
Reaction score
5,043
Kwanza niwasalimu kwa jina la muungano wa Tanzania.

Bila kupoteza wakati niende moja kwa moja kwenye mada, Rais wetu mama samia Kama unavyojua mwaka mmoja baada ya hayati JPM kuingia madarakani 2016, kwa kushirikiana na wizara ya maliasili na utalii chini ya jumanne maghembe alipiga marufuku ya usafirishaji wa viumbe hai njee ya nchi.

Raisi JPM alitumia mgongo wa kulinda rasilimali za nchii akapiga marufuku hii biashara huku akijua iko halali kisheria, Serikali ilichokifanya Ilienda ikazuia mamilioni ya pesa za wafanya biashara ambazo walikuwa wamelipwa kutoka mataifa ya njee, haikuishia hapo ikaenda ikakamata na kuzuia wale viumbe, na ilihali serikali ilikuwa imesha chukua kodi za kukamata hao wanyama.

Mama samia kama unavyojua hawa viumbe hai ambao serikali iliruhusu wafanya biashara wawauze njee ya nchi, hawana muingiliano wowote na wanyama wetu wanaopatikana kwenye hifadhi za taifa, wanyama waliokuwa wanasafirishwa niwale wanaopatikana kwenye mazingira yetu ya kila siku.

Kuna viumbe kama jongoo, vinyonga, vipepeo, ndege waharibifu, nyoka, mijusi, konokono,panya hawa viumbe wote watanzania wengi walikuwa wanafaidika nao pia Government ilikuwa inapata kodi kubwa,,ukamataji wa hao viumbe ilikuwa ni ajira kwa watu wengi, hata kwenye vitalu vya kuwalisha watanzania wengi walikuwa wameajiriwa huko.

Kubwa zaidi hii biashara ilikuwa ni chanzo kikubwa cha fedha za kigeni, Magufuli pamoja na Kigwangala walihakikisha wanaharibu kila kitu, walipora mitaji, wakaharibu zoo za wafanyabiashara, wakazuia ukamataji, wakapora vibali, jambo ambalo lilisababisha wafanya biashara kupoteza wateja wa kudumu kutoka mataifa ya ulaya na America.

Jambo la kusikitisha na kufedhehesha nchi majirani mfano Kenya ndio zimatake over hii biashara ,wazungu wote waliokuwa wanachukua mzigo kutoka Tz now, wanaeda kwa majirani zetu kenya na uganda, Mbaya zaidi kuna ndege huwa wanahama kwa misimu kwenda Kenya then wanarudi tz, wakienda kule hukamatwa, wakirudi huku sisi tunawaacha.

Wizara ya Maliasili kila mwaka hupoteza mabilioni kukodi ndege zakumwaga dawa za kuuwa ndege waharibifu, ambao hao hao tungeweza kuwakamata na kuwauza serikali ikapata kodi.

Mama yetu mama Samia uchumi umetetereka sana hata hiyo 4.8 nadhani ni uongo, uchumi umeyumba haiwezekani mtu unakosa hata 2000 ya nauli huku jongoo wamejaa pale jangwani na jongoo mmoja ni dola 1.2, kuna vipepeo wanafika hadi dola 10 za Kimarekani.

Mama tunaomba uliangalie hili swala kwa jicho la tatu maana huu uonevu wakati unafanyika nawewe nae ulikuwa unaotazama.

Halafu serikali ikawa inasema wanasema wanatoa vibali vya kukamata ila kwa maonesho ya ndani ya nchi mtanzania gani ataoa hata 100 aendee kuangalia nyoka au vipepeo.
 
Back
Top Bottom