Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,170
- 6,757
Wanabodi ni wazi kabisa pamoja na kuwa tuko kwenye msiba mkubwa kitaifa lakini bado kuna tofauti kubwa na chuki ndani ya jamii yetu.
Ni katika utawala wa awamu ya tano ile ngwe ya kwanza kulitokea sintofahamu ambazo kwa ujumla zilileta kilio na maumivu katika jamii yetu. Maana kuna watu walipotea mpaka leo hatujui wapo wapi.
Zipo maiti ziliokotwa katika fukwe za bahari na mto ruvu. Pia kuna watu wengi ambao ndugu zao wanadai walipoteza maisha wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola hususani polisi. Pia tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi lilileta hofu na chuki kubwa.
Leo alipomaliza kuhutubia rais Samia Suluhu ameligusia juu ya kuanza upya na kuacha togauti na chuki zilizopo. Maana mpaka anasema hivyo lazima atakuwa amepewa taarifa kuwa chuki na tofauti zipo
Sasa je, watanzania waliopoteza ndugu zao, waliojeruhiwa , na ambao walipoteza haki zao mpaka kunakuwa na chuki rais wetu mpya anawasaidia vipi? Au ndio imetoka?