Rais Samia, tafadhali usianzishe mchakato wa Katiba mpya mpaka ujiridhishe usimamizi wa mchakato huu

Rasimu ya Jaji Warioba hiyo hatua ilishapita. Hatua iliyopo ni Katiba pendekezwa kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura ya maoni.
Tuanze afresh au tukaipigie kura Katiba pendekezwa. Kurudi kwenye hatua iliyokwisha pita ni unconstitutional kwa maoni yangu.
 
Sawa mkuu wangu nimeridhia unipinge.....πŸ‘

Mkuu unaihitaji katiba ya serikali tatu?!!!

TANGANYIKA tuliyoizika 6 feet under the ground IFANYIWE maombi na dua ifufuliwe mkuu?!!!!
Kwa kweli mimi naonelea ni bora tuwe na serikali 3. Muundo wa serikali mbili dhamira yake ilikuwa ni kuimeza Zanzibar na hilo halikubaliki ndugu.

Wacha Tanganyika ifufuke
 
Mkuu bunge lilivurugika, hatukufikia hata hatua ya kutoka na hiyo katiba pendekezwa ya kupelekwa kwa wananchi
 

Mkuu kwa taarifa yako, katiba hii iliyompa rais ya madaraka karibu sawa na Mungu, ilitungwa na watu chini ya hao 100. Pitia vizuri rasimu ya Warioba, sehemu kubwa imesimamia maoni ya wananchi, na sio ya kikundi cha watu wachache wenye uchu wa madaraka.

Kwenye bunge lile la katiba kama sio kugeuza bunge lile la kawaida na kuwa ndio bunge la katiba, huku likijaziwa na watu kadhaa, leo hii tungekuwa na katiba bora kabisa, na ingefuatwa tu, kwani hata hii ya sasa sio wote tunakubaliana nayo, bali tunashurutishwa kuitii.

Kwahiyo usipate shida na malalamiko ya baadhi ya watu, kwani hiyo ni dalili kuwa watu wanafikiri, ila tutaipima katiba hiyo kwa ubora wake kulinganisha na ya sasa. Hili jambo la katiba mpya sio gumu, bali waovu wengi hasa walioko madarakani, hawaitaki maana haiwapi nafasi ya kuendelea kukaa madarakani kwa shuruti. Kundi hilo la waovu wachache wanaichukulia katiba mpya kama nyaraka ya uchaguzi. Ila nijuavyo katiba mpya itapatikana tu, ni vyema ipatikane sasa tukiwa na amani, na sio kwa hali ya machafuko
 
Mkuu bunge lilivurugika, hatukufikia hata hatua ya kutoka na hiyo katiba pendekezwa ya kupelekwa kwa wananchi
UKAWA walitoka, Bunge liliendelea mpaka mwisho. Hukumbuki Mwanasheria Mkuu wa SMZ ambe ndie Makamo wa Kwanza wa RAIS kwa Sasa alipotimuliwa kwa kupiga kura kinyume na matakwa ya mwajiri wake?
Hukumbuki shutuma zilizotelewa kwamba mpaka watu waliofariki walipiga kura (mama yake Zitto) na watu waliokuwa nje ya nchi (Mohamed Raza- alikuwa Hija).
Kama hii hatua iliyopo haikubaliki Sheria ya mchakato ibadilishwe au ifutwe au watu wafungue kesi ya kupinga mchakato wa jinsi hatua ya Katiba pendekezwa ilivyofikiwa.
 
Kwa kweli mimi naonelea ni bora tuwe na serikali 3. Muundo wa serikali mbili dhamira yake ilikuwa ni kuimeza Zanzibar na hilo halikubaliki ndugu.

Wacha Tanganyika ifufuke
Akhui unanifurahisha kwa UZALENDO KUNTU moyoni mwako.....

Sawa ninaelewa mantiki ya hoja yako Al akhui muadhama!!!

Ila langu ni hofu tu ya hizo serikali 3....
Hofu yangu si Zanzibar....laa hashaa...

Hofu yangu ni kwetu huku "Mrima".....

Mkuu wako "wanamrima" wenzangu wasiupenda Muungano....
Wako "wanamrima" wenzangu wasiowapenda WAZANZIBARI....wana ajenda za SIRI ZA KUWABAGUA hivyo "walivyo WAZANZIBARI".....

Kwao hawawaangalii Wazanzibari kuwa ni WANDENGEREKO ,WAMWERA ,WAMAKONDE ,WAMATUMBI ,WANYAMWEZI NA WANGINDO waliohamia visiwani miaka tele nyuma.....

Uhafidhina wa baadhi ya "wanamrima" hao huwapelekea kuwaona WAZANZIBARI kuwa kama wenye asili ya kutoka mbali kabisa na visiwa vya "MADAGASCAR".....JAMBO AMBALO SI KWELI HATA....!!!

Hoja yangu iko kwao....ikitokea serikali 3 hawa hawana Cha KUPOTEZA.....hawaihitaji Zanzibar....watakuja na RAI YA KUUVUNJA MUUNGANO....mkuu walipata kutokea Hawa ....wale G55.....

Binafsi kama kijana ninajisikia unyonge sana IKITOKEA wanamrima TUTENGANISHWE NA MAKUNDUCHI...."mwakakogwa"🀣

TUTENGANISHWE na PEMBA NA CHOKOCHO.....

Mkuu wangu TUYAFIKIRIE NA HAYO mkuu.......

#StaunchSupporterOfSSH
#DieHardFanOfCCM
#KaziIendelee
 
Mkiendelea kushupaza shingo sisi tutamlilia mwenyezi Mungu tutamsihi aingilie kati kwa jinsi aonavyo yeye inafaa ili watanzania wapate haki zao.
 
Kwani walioua huo mchakato si hao hao fisiemu, mbona tunachoshana.....
 
Hakika πŸ˜„ Natakiwa kuwa ndani ya jengo kutoa mapendekezo mbalimbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…