Inaonekana Watanzania karibu wote tuna msimamo mmoja juu ya kuanza upya au kuendelea na rasimu ya Jaji Warioba. Hili inawezekana lipo clear already.
Hapo kwenye hao watu wa kushiriki kwenye bunge la katiba sasa ndio balaa lipo hapo. Na ndio maana nkasema, Mheshimiwa Rais asiuanzishe mchakato huu mpaka apate watu wa kuaminika ambao hawatatutia hasara kama taifa kama ilivyotokea kipindi kile.
Huu mchakato ni mgumu sana jamani na kuthibitisha hilo, wengi wetu hatuwezi kuipanga safu ambayo inaweza ikaitwa bunge la katiba.
Leo nikikwambia mkuu
tindo upendekeze majina ya watu ambao wanatakiwa wawepo katika hayo makundi uliyoyataja naamini hutoweza. Kwa mfano, pendekeza hao polisi wawili, askari magereza wawili, uhamiaji wawili viongozi wa dini 16 wafugaji watano wakulima watano (huku ukijua Sumry nae na mkulima
😀 😀 😀 😀 )
Hao wanasiasa 20 mkuu utazua balaa kubwa hapo na majina utashindwa kuja nayo.
Kiufupi hao watu mia wakichaguliwa basi yatazuka makubwa kwamba katiba ni ya hao watu 100 na sio ya Watanzania.
Kwenye wanamichezo tafadhali ndugu yangu
isajorsergio asikose.