Rais Samia: Tanzania haiwezi kupatwa na janga la njaa. Tuna akiba ya tani laki 1.5 za Chakula kwenye Ghala la Taifa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Jubilei ya Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dares Salaam tarehe 11 Septemba, 2022

HISTORIA FUPI YA WAWATA

Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) ni umoja ulioanzishwa mwaka 1972 ukiwa na jukumu la kuwaweka wanawake pamoja katika kutatatua changamoto zinazowakabili za kiroho na kimwili kwa kushirikina na Kanisa Katoliki Tanzania.

Ni mwamvuli wa ushirika wa pamoja kwa wanawake wakatoliki Tanzania.

Halfa hii ya kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwake imehudhuriwa na wanawake wakatoliki kutoka majimbo yote 34 ya Tanzania, Maaskofu, viongozi wa kanisa katoliki, Watawa, wawakilishi wa Dini na Madhehebu mengine pamoja na watu wengine wenye mapenzi mema.

====

Askofu Gervas Nyaisonga - Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)

Serikali imekuwa na sera wezeshi zinazo wafanya wanawake kupambana na hali zote ngumu za nchi yetu. Katika awamu zote 6 za uongozi wa nchi yetu, wanawake wamekuwa mstari wa mbele kwenye nyanja zote.

Ukimuwezesha mwanamke mmoja unakuwa umewezesha kundi kubwa. Tunaomba serikali iendelee kuwezesha wanawake kwani wakipewa fursa watakuwa tayari kizitumia karama zao vizuri, hii ni faida kubwa kwa Taifa letu.

Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mafanikio ya wanawake wakatoliki (WAWATA) yameonekana kupitia kauli mbiu ya Kutumika na kuwajibika. Umoja huu unao umuhimu wa kipekee.

Hongereni kwa kujikita katika Malezi ya familia na kujali watu wenye uhitaji maalumu kama wafungwa, wagonjwa, wazee, yatima na wale wenye ulemavu. Nimefarijika kusikia kuwa katika safu ya uongozi wenu kuna hadi viongozi wa kisiasa. Mnafanya vizuri sana.

Nimetiwa moyo na program ya WAWATA chipukizi. Hawa ni wamama wa kutegemewa miaka ijayo.

Katika kufungua microfinance yenu, Serikali itatoa msaada wote kuhakikisha hili linatimizwa kwa haraka.

Serikali inafurahi kuona mnashirikiana na madhehebu mengine katika kukabiliana na changamoto zenu. Changamoto ya mwanamke mmoja Tanzania ni changamoto ya wanawake wote.

Ukitaka kutoa sadaka, toa sadaka inayoendelea. Hongereni kwa kupanda miti 530,416 ambayo ni zaidi ya lengo lenu la kupanda miti 34,000 nchini. Hii ni sadaka inayoendelea kwani mazingira yetu ni muhimu kwa uhai.

Malezi ya watoto yakaziwe. Kuna maporomoko ya maadili kwa watoto na vijana wetu. Mwenyezi Mungu anasema “enyi watoto mmetokana na Mungu, yeye amewalinda…..” Wanawake tumepewa jukumu la kusimamia malezi ya watoto. Inafaa wawe waadilifu na wenye tabia njema.

Mwanamke hufungua mdomo wake kwa hekima na nidhamu. Pia, wanawake ni jeshi kubwa. Jeshi maana yake kulinda himaya, kulinda kilicho chako. Tunapaswa kulinda vijana wetu, tulinde watoto wetu.

Wanawake tunatakiwa kuwa jasiri na tusikate tamaa sababu Mungu yupo nasi. Mwanamke amevishwa nguo ushupavu na thamani, tusiogope.

Wanawake ndiyo tunalia sana kunyanyaswa na wanaume, lakini wanaume wananyanyasika pia. Tuendelee kuhimizana, unyanyasaji haufai kwa wote.

Ni muhimu pia kufuatilia matumizi ya vifaa vya kidijitaji (ki eletroniki) vya watoto wetu ili kufahamu wanafanya nini huko kwani vinaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa maadili.

Tanzania bado ina hali nzuri ya akiba ya chakula. Tuna tani laki moja na nusu kwenye ghala la chakula la Taifa. Akiba hii inatufaa watanzania, inaweza kuzuia tusiingie kwenye janga la njaa.

Serikali pia inatoa ruzuku kwa wakulima ili wahimili kulima mazao mengi. Tuombe Mungu tupate mvua za kutosha.

Kuhusu bima ya afya kwa wote, Bunge lijalo litaputisha sheria hii hivyo kila Mtanzania atanufaika nayo.

Tanzania ni nchi nzuri. Tuna mambo mengi ya kujivunia, tunaweza kufanya biashara popote kupitia bandari ya Dar es salaam, tuna maziwa, mito na ardhi yenye rutuba kubwa. Tuna madini ambayo mengine hata hatujui majina yake. Tatizo ni namna gani ya kutumia.

Matumaini yangu, miaka 50 ijayo Tanzania iwe na jamii inayoweza kutumia rasilimali hizi kwa ufanisi na manufaa makubwa.

Twendeni kuchapa kazi, tuijenge Tanzania yetu. Kila lakheri kwa WAWATA na kanisa lote kwa ujumla.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Jubilei ya Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dares Salaam tarehe 11 Septemba, 2022

HISTORIA FUPI YA WAWATA

Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) ni umoja ulioanzishwa mwaka 1972 ukiwa na jukumu la kuwaweka wanawake pamoja katika kutatatua changamoto zinazowakabili za kiroho na kimwili kwa kushirikina na Kanisa Katoliki Tanzania.

Ni mwamvuli wa ushirika wa pamoja kwa wanawake wakatoliki Tanzania.

Halfa hii ya kuadhimisha miaka 50 ya kuanzishwa kwake imehudhuriwa na wanawake wakatoliki kutoka majimbo yote 34 ya Tanzania, Maaskofu, viongozi wa kanisa katoliki, Watawa, wawakilishi wa Dini na Madhehebu mengine pamoja na watu wengine wenye mapenzi mema.

====

Askofu Gervas Nyaisonga - Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)

Serikali imekuwa na sera wezeshi zinazo wafanya wanawake kupambana na hali zote ngumu za nchi yetu. Katika awamu zote 6 za uongozi wa nchi yetu, wanawake wamekuwa mstari wa mbele kwenye nyanja zote.

Ukimuwezesha mwanamke mmoja unakuwa umewezesha kundi kubwa. Tunaomba serikali iendelee kuwezesha wanawake kwani wakipewa fursa watakuwa tayari kizitumia karama zao vizuri, hii ni faida kubwa kwa Taifa letu.

Samia Suluhu Hassan - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mafanikio ya wanawake wakatoliki (WAWATA) yameonekana kupitia kauli mbiu ya Kutumika na kuwajibika. Umoja huu unao umuhimu wa kipekee.

Hongereni kwa kujikita katika Malezi ya familia na kujali watu wenye uhutaji maalumu kama wafungwa, wagonjwa, wazee, yatima na wale wenye ulemavu. Nimefarijika kusikia kuwa katika safu ya uongozi wenu kuna hadi viongozi wa kisiasa. Mnafanya vizuri sana.

Nimetiwa moyo na program ya WAWATA chipukizi. Hawa ni wamama wa kutegemewa miaka ijayo.

Katika kufungua microfinance yenu, Serikali itatoa msaada wote kuhakikisha hili linatimizwa kwa haraka.

Serikali inafurahi kuona mnashirikiana na madhehebu mengine katika kukabiliana na changamoto zenu. Changamoto ya mwanamke mmoja Tanzania ni changamoto ya wanawake wote.

Ukitaka kutoa sadaka, toa sadaka inayoendelea. Hongereni kwa kupanda miti 530,416 ambayo ni zaidi ya lengo lenu la kupanda miti 34,000 nchini. Hii ji sadaka inayoendelea kwani mazingira yetu ni muhimu kwa uhai.

Malezi ya watoto yakaziwe. Kuna maporomoko ya maadili kwa watoto na vijana wetu. Mwenyezi Mungu anasema “enyi watoto mmetokana na Mungu, yeye amewalinda…..” Wanawake tumepewa jukumu la kusimamia malezi ya watoto. Inafaa wawe waadilifu na wenye tabia njema.

Mwanamke hufungua mdomo wake kwa hekima na nidhamu. Pia, wanawake ni jeshi kubwa. Jeshi maana yake kulinda himaya, kulinda kilicho chako. Tunapaswa kulinda vijana wetu, tulinde watoto wetu.

Wanawake tunatakiwa kuwa jasiri na tusikate tamaa sababu Mungu yupo nasi. Mwanamke amevishwa nguo ushupavu na thamani, tusiogope.

Wanawake ndiyo tunalia sana kunyanyaswa na wanaume, lakini wanaume wananyanyasika pia. Tuendelee kuhimizana, unyanyasaji haufai kwa wote.

Tanzania bado ina hali nzuri ya akiba ya chakula. Tuna tani laki moja na nusu kwenyr ghala la chakula la Taifa. Akiba hii inatufaa watanzania, inaweza kuzuia tusiingie kwenye janga la njaa.

Serikali pia inatoa ruzuku kwa wakulima ili wahimili kulima mazao mengi. Tuombe Mungu tupate mvua za kutosha.

Kuhusu bima ya afya kwa wote, Bunge lijalo litapitisha sheria hii hivyo kila Mtanzania atanufaika nayo.

Tanzania ni nchi nzuri. Tuna mambo mengi ya kujivunia, tunaweza kufanya biashara popote kupitia bandari ya Dar es salaam, tuna maziwa, mito na ardhi yenye rutuba kubwa. Tuna madini ambayo mengine hata hatujui majina yake. Tatizo ni namna gani ya kutumia.

Matumaini yangu, miaka 50 ijayo Tanzania iwe na jamii inayoweza kutimia rasilimali hizi kwa ufanisi na manufaa makubwa.

Twendeni kuchapa kazi, tuijenge Tanzania yetu. Kila lakheri kwa WAWATA na kanisa lote kwa ujumla.

Chadomo wanasema anachukiwa Sana mitaani 😁😁
 
Rais kushiriki kwenye hafla kama hizo kutokana na cheo chake ni dalili ya kupendwa? Labda useme hafla anazoshiriki rais, kigezo ni kiwango chake cha kupendwa.
 
Kwa nini umualike mtu anayechukiwa? Si umualike anayependwa?

Kwa hiyo event ya Sugu kule Dar Rais alishiriki kwa cheo chake?

Utashangaa 2025 hata Lissu akampa kura SSH maana kamsitahi Sana.
 
Unamualika anayependwa au anaalikwa mwenye mamlaka? Kwenye hafla za kitaasisi mara nyingi waalikwa ni viongozi haswa wa serikali. Kwenye fiesta ndio hualikwa msanii anayeng'aa kwa muda huo. Hili halihitaji degree kulifahamu.
 
Nimeishi majimbo mengi ila sijaona wala kusikia jimbo ambalo WAWATA yake ni very active kama Jimbo Katoliki la Bukoba. Ile WAWATA achana nayo kabisa
 
Ni lini Tanzania iliwahi kuwapa wananchi wake chakula ?
Leo tuna uziwa maharage 3500/ bado ana sema hatuta kufa njaa. Ni Mtanzania gani wa kawaida ana weza kununua kilo mbili ya mchele kwa 6000/ au unga kwa 1800 na ana watoto sita?
 
Back
Top Bottom