One who respects power does not fear it. Before Magufuli, nchi ilikuwa imekaa kama genge la wahuni wachache. Don't forget that. JPM kabadili upepo wa mazoea mabovu. Heshima na nidhamu ya kazi. Miradi ya maendeleo. Utu wa Mtanzania. Kujitegemea na kutotegemea misaada ya mataifa mengine. Rasilimali za nchi kwa ajili ya taifa. Vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali za umma. ^Mahali tulipofika kama nchi, tunamhitaji kiongozi madhubuti kama JPM^ ~ ilisikika sauti kutoka upinzani.
Naona unataja baadhi ya mengi niliyofurahia kayafanya, hata kama aliyafanya kwa njia za hovyo. Napenda uelewe hivyo, na pengine kama ungefuatilia ninayoandika hapa JF baada ya Magufuli kuondoka na mama kuingia utaona ni kama nilikuwa mfuasi wake mkubwa.
Hapana. Yale aliyofanya nimkatae, na kusema kweli nimchukie, yalifuta kabisa haya mazuri uliyoorodhesha hapa.
Asingejihusisha na yale mabaya yake, Magufuli angekuwa rais mzuri sana kumkaribia Mwalimu. Lakini tabia zake na udhaifu wake (sijui ni ubinaadam wake) ulimfanya awe kiongozi wa hovyo kabisa (as far as I am concerned).
Na ndiyo maana unaona hayo maneno kwenye 'signature' yangu: "One who respects power does not fear it." Niliyaandika maksudi siku moja baada ya kuchukizwa sana na vitendo vya uonevu alivyokuwa akifanya Magufuli.
Huyu mama angeweza kuyafanya, au kuyaacha yaendelee hayo mazuri ya Magufuli bila ya upande mbaya wake, na akajiepusha na makundi ya mtu wa Msoga, kazi yake ingekuwa nyepesi na nzuri.
Lakini inaelekea mama tayari amekwishatekwa huyu, anachukua na kuendeleza alipoachia Kikwete.
Tutakuwa na hali ngumu sana.
Kwa hiyo, Bwana Jasmoni Tegga, nielewe ninaposimamia mimi. Usinirundike tu kwenye kundi. Nina mawazo ninayoyasimamia mwenyewe, nilishavuka hatua ya kufuata mkumbo.
Niliyoandika hapo juu na wewe ukani'quote', ndio uamini wangu haswa. Magufuli aliharibu sana kwa tabia zake mbaya.