CCM Music
JF-Expert Member
- Dec 5, 2018
- 1,036
- 1,784
Nasema irudiwe na irudiwe tena na tena.
Huyu mtalaam lazima atakuwa mwanaCCM kindakindaki maana haya ndo mawazo chanya ya wana CCM.
Twende pamoja.
CCM CCM CCM nimewaita mara tatu. Mpeni usajili huyu mwamba tena jezi namba 9 striker kabisa tumalize mechi zetu mapemaaaaa.
=========
USAFI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM – TANZANIA
(Kumradhi Mama, naomba niandike kwa lugha za vijana wa mitandaoni)
Mama Shikamoo!
TUFUATE UTARATIBU HUU, JIJI LA DSM LITAKUWA SAFI KILA SIKU
Kila eneo DSM lina mmiliki wake. Kila kiwanja DSM lina mmiliki wake. Kila kitu DSM kina mmiliki wake. Sasa tufuate utaratibu huu kuhakikisha kuwa Jiji la DSM linakuwa safi kila siku.
Kila mwenye eneo DSM ahakikishe kuwa eneo lake linakuwa safi kila siku
Kila anayetumia eneo Jijini DSM kwa shughuli zake zozote zile ziwe za kiuchumi, ama kwa chochote kile hata kama kinatumika kama kijiwe cha kupiga stori za Simba na Yanga ahakikishe kuwa eneo lake linakuwa safi kila siku.
Mjumbe wa eneo husika anapaswa mara kwa mara kuangalia usafi wa maeneo yake anayosimamia kama Mjumbe na kutoa taarifa fupi kwenye Kitengo husika cha jiji kuhusu hali ya usafi wa eneo lake.
Jiji la DSM liunde kitengo maalum cha kuhusika na usafi wa Jiji la DSM. Kitengo hiki kiwe na mawasiliano ya kila Mjumbe kwenye maeneo yote DSM kwa ajili ya kupata brief za mara kwa mara kuhusu usafi wa eneo husika.
Katika jiji la DSM kuwepo na namba za simu sehemu zote za Jiji la DSM kwa ajili ya mtu yeyote kuweza kuripoti uchafu kwenye eneo husika katika Jiji la DSM. Namba hizo ziwe ni za Kitengo cha Usafi wa Jiji la DSM.
Kuwepo na faini ya mtu anayekutwa na uchafu kwenye eneo lake. Faini isiwe ya kukomoana ama isiwe ya kuchonganisha wananchi na Serikali yao.
Kitengo cha usafi wa Jiji la DSM kiwe na watu wenye weledi wa kutosha, hekima na busara na wasiofanya kazi kwa mihemuko ya kuwaumiza ama kuwatesa wananchi bali wafanye kazi yao ya kusimamia Usafi wa Jiji kwa weledi wakiwa na nia ya kusaidia Serikali na sio kuchonganisha Serikali na wananchi kwa maamuzi yao ya kimhemko.
Mara nyingine kuna maeneo ambayo umiliki wake ni wa umma, mfano bara bara za mitaa ama viwanja vya wazi. Hiki kifanyike:
Kama ni barabara mfano ya mtaa. Wananchi wanapaswa kugawana barabara hiyo katikati. Yaani kila mmoja anapaswa kuhakikisha kuwa kunakuwa kusafi kule upande ambao anapakana nao kwa kuanzia katikati. Yaani, inakuwa kama wamegawana katikati. Utaratibu huu utumike hata kwa viwanja vya wazi.
Hata hivyo, watu wa DSM hawana utamaduni wa kutupa takataka hovyo sehemu za viwanja vya wazi ama barabara za mitaa. Lakini ni vema utaratibu huu ukawepo.
GHARAMA ZA UENDESHAJI WA KITENGO HIKI:
Ni wazi hakuna gharama kubwa sana, cha muhimu ni utashi tu. Ila hiki kifanyike ili kuepusha Serikali kubeba gharama: Magari yote ya taka, ama kampuni zote za taka zinapaswa kuchangia gharama kidogo kwa ajili ya uendeshaji wa kitengo hiki. Ikumbukwe pia kuwa wao ndio wanufaika wakubwa wa huduma za kitengo hiki.
# Suluhu is the legacy of Samia.
# New Tanzania – Tanzania Mpya ya Samia.
Wasalaam,
ONE VOTE COUNTS TANZANIA (IDARA KUU HUDUMA KWA WANANCHI–TANZANIA). Twitter: ovctanzania, Instagram: ovctanzania, Email: ovctanzania@gmail.com SIMU: +255 (0) 785 29 45 45.