Rais Samia: Tumeongeza shilingi 100 katika kila lita ya mafuta ili tuweze kukusanya fedha zitusaidie kujenga Barabara za Vijijini

Rais Samia: Tumeongeza shilingi 100 katika kila lita ya mafuta ili tuweze kukusanya fedha zitusaidie kujenga Barabara za Vijijini

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1625762525798.png

Akiwa anamalizia siku ya pili ya ziara yake Mkoani Morogoro Rais Samia ametoa ufafanuzi juu ya ongezeko la bei ya mafuta ambalo limekuwa likijadiliwa na wengi mitandaoni

Katika hili Rais Samia amesema “Tumeongeza fedha kidogo kwenye mafuta, mtakuwa mmesikia kelele za mafuta. Tumeongeza shilingi 100 katika kila lita ya mafuta ili tuweze kukusanya fedha zitusaidie kujenga barabara za vijijini [TARURA]."-
 
Tujengee mama, hizi halmashauri ziko hoi hazijiwezi. Na maji pia vijijini ni shida
 
Na wakaongeza kodi kwny Simu huko ikiitwa ni kodi ya uzalendo.
 
Katika upande mwingine Rais amevunja ukimya wa sababu ya bei ya mafuta kupanda nchini akisema ni mkakati wa Serikali kuongeza fedha kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili kuimarisha ujenzi wa barabara hizo.

“Nataka niwape taarifa kwamba tumeongeza fedha kidogo kwenye mafuta. Pengine mmesikia kelele za mafuta, lakini tumeongeza Sh100 katika kila lita ya mafuta ili tuweze kukusanya fedha zikatusaidie kujenga barabara za vijijini”- amesema Rais Samia.

Aidha Rais amefafanua kuwa fedha nyingi zimepotea katika ujenzi na ukarabati wa barabara ambazo zimekuwa zikiharibiwa na mvua.
 
Back
Top Bottom