Katika upande mwingine Rais amevunja ukimya wa sababu ya bei ya mafuta kupanda nchini akisema ni mkakati wa Serikali kuongeza fedha kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili kuimarisha ujenzi wa barabara hizo.
“Nataka niwape taarifa kwamba tumeongeza fedha kidogo kwenye mafuta. Pengine mmesikia kelele za mafuta, lakini tumeongeza Sh100 katika kila lita ya mafuta ili tuweze kukusanya fedha zikatusaidie kujenga barabara za vijijini”- amesema Rais Samia.
Aidha Rais amefafanua kuwa fedha nyingi zimepotea katika ujenzi na ukarabati wa barabara ambazo zimekuwa zikiharibiwa na mvua.