Rais Samia, tunakusubiri kwenye U-DAS na Watumishi wa Umma

Nafasi ya DAS=Nafasi ya kiutendaji lazima mtumishi awe na uzoefu na taratibu za Utumishi wa umma unaozingatia sheria,kanuni na taratibu.
Nafasi ya DED=Nafasi ya kiutendaji lazima mtumishi awe na uzoefu na taratibu za Utumishi wa umma unaozingatia sheria,kanuni na taratibu.

Katika nafasi hizo hapo juu,ndipo maana ya utawala bora inapopatikana,na awamu hii inataka kurekebisha makosa yaliyojitokeza hapo nyuma(maana mtawala yule hizo nafasi mbili aliwapa makada,wakajikuta wateuliwa wote wana uchu wa nafasi za kisiasa,na wengi wao walikuwa hawajui taratibu za kiserikali) na kufanya eneo la utawala kuwa na malumbano yasiyo isha,na kutunishiana misuli.Kwa kweli tulicheleweshewa maendeleo!
 
Acha kabisa JPM aliharibu ila huyu anadhirisha kuwa yeye na mwendazake ni kitu kimoja
 
Sifa ni kuw mtz mchapakazi mwaminifu na mzalendo na pia mwelevu siyo lazima awe public servant mkuu!
Huna unalolifahamu mkuu. Kuna tofauti ya vyeo vya kiutendaji na vya kisisasa ndio maana migogoro imejaa maana unateua Mwandishi kuwa DED unategemea nini (Ref DED wa MBULU)
 
Shida ndio ipo hapo , JPM mlisema hashauriki na huyu nae hivyo hivyo?? Mbona sheria zipo wazi tu
 
Walio kwenye sekta binafsi wao vipi?? Hawana nafasi?
 
Asante mkuu[emoji1756][emoji1756][emoji1756]
 
Hadi mtangazaji wa shilawadu angeweza kuteuliwa DED, hali ilikuwa ya kukatisha tamaa kwa watumishi wa umma...
Wajinga WALIBAKA na WANABAKA Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma
 
Subiri mshtuko😜! Mamlaka aliyonayo rais wetu hayamfungi hivyo akiamua vinginevyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…