Rais Samia tunaomba ingilia kati suala la mitandao

Abu Ubaidah Commando

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
7,591
Reaction score
6,946
Bandugu kwema?

Kama kichwa cha habari kinavosomeka apo juu, naomba mh Rais aingilie kati suala hili otherwise tutasusia ama kuandamana.

Wamepunguza MB gharama imebakia ileile ya mwanzo, maana yake nini kutukomoa ama ninii!!! Kana vipi na gharama za kununua vifurushi zipungue.

Hii siyo haki aisee, nimeruka mkojo nakanyaga maavi(nimehama Tigo sababu ya vifurushi kupanda bei na mtandao kukwamakwama, clips zinatake time kufunguka, nimehamia haloteli nako nikadhani kuna unafuu upande wa internet kama ilivyo apo mwanzo,,,aisee nimejiunga GB za kutosha bandugu, dakika chache and internet iko very very slow, inakwama, nilikuwa nacheki game ya Spain na Italy mwishoe nikaamua kughaili tu 😡

Halotel na mitandao yote Mungu anawaona. Nikisema nirudi Tigo nakutana na bei kubwa za vifurushi, dahh akili imesizi hapa.


MUHESHIMIWA RAIS INGILIA KATI SUALA HILI.
 
Hii ni sawa na kupikwa mgumi na John halafu unakwenda kumuomba baba John amwambie mwanawe awache kupiga wenziwe. Baba John anamwambia mwanawe kesho uwa na kabisa wakujuwe wewe kidume cha mbegu mimi sijaza ngese.(Mama anasema kaza hapohapo)



Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Hapa dawa ni kuandama tu sisi ni vijana wa kizazi kipya lazima tuchukue maamuzi,tukiachana na maswala ya vifurushi kuwa ghali kuna mahitaji mengine muhimu ya binadamu kama mafuta ya kula yamepanda mara bili zaidi ya hapo awali.maisha yamekuwa magumu sana tofauti na hapo awali na serikali ipo kimya tu. Nini maana ya kuwa kiongozi? Sisi wananchi tunateseka huku
 
Ukishawaelewa Watanzania unabaki tu kustaajabu kuwa kuna watu waoga na wanyonge kama hawa duniani tena ambao hawaishi misituni bali wana access na dunia inavyokwenda.

Aliyetupumbaza anahitaji kupewa Nobel Peace Prize maana labda ameepusha maafa mengi.
 

Inackitisha mno mkuu. Kungerikuwaa na WIFI za kutembeanazo safii. Tungeachana na izo takataka zao.
 

Kweli chief,,uko sahihi
 
Labda kuna amri wamepewa wapunguze ili kupunguza wanaoipa makavu serikali, huu ni uhuni haukubaliki, internet wengi wanaingia huko kupata taarifa wanazozihitaji, siyo siasa tu
 
Kama hawa vodacom wametoa kabisa kifurushi cha GB moja pamoja na muda wa maongezi.Yaani haya makampuni ya kutoa huduma yanaona internet ni anasa wakati ndio yanatakiwa yatoe zaidi yenyewe yanapunguza
 
Mi naona gharama zingeongezwa mara dufu ili tutoke kwenye uchumi wa kati tuingie uchumi wa juuu 🤣🤣🤣

Km hutaki hamia Burundi kwenye unafuu🤣🤣🤣
 
Pia hili swala la facebook, instagram na WhatsApp aliangalia maana zina zima pasipo taarifa
 
Mkuu, wewe hauoni kuna collusion? Haiwezekani makampuni yote yafanye jambo moja la hovyo kwa wakati mmoja kama hivi. Gharama zimeongezeka kuliko uhalisia wa maisha ya Watanzania (na hakuna sababu yoyote ya msingi ya ongezeko hili la gharama na kuwekwa vifurushi vya ajabu ajabu) na wanatunyima fursa ya kupashana na kupata habari.

Faida za kutumia mabilioni ya fedha zetu kuwekeza katika mifumo ya internet ikiwemo mkongo wa Taifa ni nini kama internet yenyewe inaenda kuminywa ili tusiitumie ipasavyo?

Kwanza hii collusion ipo kati ya makampuni haya na serikali. Wengine tulishaiona hii tukaiita kwa jina lake sahihi, Ufashisti.
 
Ndio maana wananchi wa nchi hii wataendelea kutawaliwa milele. Yaani uandamane sababu vitu vidogo sana hivyo?. Swala la internet ndio uandamane?. Linaloathiri unakuta 15% au 10 au chini ya hapo tu ya watanzania wote.

Uache kuandamana sababu ya katiba?. Uache kuandama sababu ya mafuta kupanda?. Uache kuandamana sababu ya mafisadi?. Uache kuandamana viongozi wanatibiwa nje mabilioni ya pesa (spiker),ingali wananchi wanakosa dawa,vitendea kazi tu kwenye hospital za ndani. Uache kuandamana kiongozi anakuambia hamia Burundi baada ya kufanya vurugu kwenye miamala?. Eti uandame internet...!!
 
Karibu ttcl
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…