Rais Samia, tungependa kama ulivyokuwa mwepesi kutolea ufafanuzi suala la Ndugai, Kabudi na Lukuvi basi hata kuungua kwa Masoko kuwa pia mwepesi

Rais Samia, tungependa kama ulivyokuwa mwepesi kutolea ufafanuzi suala la Ndugai, Kabudi na Lukuvi basi hata kuungua kwa Masoko kuwa pia mwepesi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
GENTAMYCINE nawaomba tu hao 'Team Mikakati Awamu ya 6' wajitahidi kwa sasa kubadili Mbinu za Kuungua 'Kimkakati' kwa 'Masoko Makubwa' nchini kwani kwa sasa hata Mtoto Mdogo ameshajua kuwa nia ni 'Kuwakomoa' Wamachinga waliokuwa Wakipendwa na Hayati na pia kuruhusu Ujenzi mpya wa Masoko ili Watu fulani fulani wapige Pesa na pia 'Mshauri Mswahili' kupitia Marafiki na Washirika wake Kibiashara wapewe Tenda na Yeye awekeze humo humo kwa Kificho kama afanyavyo kwa Wadhamini Wakuu wa Yanga SC akina GSM.

Soko Kuu (Kubwa) la Kariakoo limeungua (ila GENTAMYCINE nasema limeunguzwa Kimkakati) tokea mwaka jana na mpaka leo Kamati haijaja na Ripoti yoyote ile.

Ila muda wa Kumkandia Ndugai wa Watu ulikuwepo na pia muda wa kurudia mara kwa mara kutolea Ufafanuzi (ambao hata hivyo wenye Akili Kubwa hatujauelewa) upo ila wa ama Kukemea hawa Wahuni (Crooks) wanaochoma Masoko Makubwa kwa Makusudi nchini au hata Kuwakamata upesi haupo.

Endeleeni tu kutufanya Sisi ni Wapuuzi.

Pia soma: Soko la Kariakoo lateketea kwa moto
 
Mataga mnateseka sana, mkuu wa mkoa, wa wilaya wakurugenzi makatibukata, kila nyanja wanafanya nini hadi rais atoe tamko au unadhan ni rais wa manzese yule?
 
Watu wameanza kupiga dili, maeneo ya wazi sasa wanajichukulia bila aibu nia wajenge shopping mall kila mahali waitwe wawekezaji
Uko sahihi tena 100% Mkuu kwani 'Mshauri Mswahili' anataka Kujenga 'Shopping Malls' za uhakika hayo Maeneo kwa Kushirikiana na Marafiki zake wa Marekani, UAE na Malaysia.
 
Rais fisadi anaehamasisha ufisadi kwenye serikali yake tena kupitia TV ya Taifa hana credibility yoyote ile ya kutolea ufafanuzi jambo lolote lile la maana,labda akaitolee ufafanuzi familia yake.
 
Sasa kama ni za Kuokoteza unapoteza muda wako wa nini kuendelea Kunisoma na Kuchangia hapa?

Kuna Watu nikiwadharau msichukie tu!!
Ni uhuru wangu kuchangia,na huu ndio mchango wangu.Kama una ngozi nyepesi hupaswi kuwa kwenye hii forum.
 
Rais aache Kazi za msingi aje. Kuzungumzia kuungua masoko? Huu ni ujinga itaonesha system imefeli,Waziri anafanya nini? RPC na Mkuu wa Mkoa Kazi yao iwe nini? PM mwenye kitengo cha maafa awe anafanya nini?
Kwahiyo Rais Kupoteza muda kila mara Kuzungumzia Suala la akina Kabudi na Lukuvi huku Wakulima nchini wakilalamika Bei ya Mbolea na Watanzania wakilalamika kuhusu Tozo Lukuki Kwako Wewe ndiyo Muhimu?

Nahisi Ubongo wako utakuwa umejaa sana 'Mchwa' hebu jitahidi ama uwapunguze au uwatoe tu Wote sawa?
 
Mataga mnateseka sana, mkuu wa mkoa, wa wilaya wakurugenzi makatibukata, kila nyanja wanafanya nini hadi rais atoe tamko au unadhan ni rais wa manzese yule?
Poor You and Hopeless.....!!!!
 
Kwahiyo Rais Kupoteza muda kila mara Kuzungumzia Suala la akina Kabudi na Lukuvi huku Wakulima nchini wakilalamika Bei ya Mbolea na Watanzania wakilalamika kuhusu Tozo Lukuki Kwako Wewe ndiyo Muhimu?

Nahisi Ubongo wako utakuwa umejaa sana 'Mchwa' hebu jitahidi ama uwapunguze au uwatoe tu Wote sawa?
Katoe funza waliojaa kwenye ubongo wako ..

Mbolea alishasema ziko njiani na zitauzwa kwa bei ya awali,unachojua ni kupinga ila hotuba ya Rais mwaka mpya hukuisikia.

Swala la kinakabudi analizungimzia kwenye hafla zinazohusu maswala ya kiutawala na hajazungimza popote tena,hiyo imetoka.

Samia tuko kazini acha kubwabwaja ujinga👇

Screenshot_20220117-094137.png

Screenshot_20220116-184917.png

Screenshot_20220116-185649.png

Screenshot_20220116-185741.png

Screenshot_20220116-185240.png
 
Back
Top Bottom