#COVID19 Rais Samia, tuondolee hili janga Wizara ya Afya. Mawaziri wako ndio kikwazo cha chanjo

#COVID19 Rais Samia, tuondolee hili janga Wizara ya Afya. Mawaziri wako ndio kikwazo cha chanjo

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Hii ni moja ya Wizara ambayo imepata mawaziri Wa Hovyo sana. Hatujui ni nini kinafanya Huyu Dr. Gwajima aendelee kufanya sarakasi zake zisizo na Tija katika Wizara nyeti kama hiyo.

Kwa nini huoni kama kuna shida? Wizara hii haihitaji Mipasho, vichekesho na Propaganda. Inataka mtu ambaye yupo serious na kazi. Huyu Waziri Gwajima Dr. Na Naibu wake hawafai. Ondoa watu hao.

Tukimwangalia huyu Waziri Gwajima na Naibu tunaona hata hizo Chanjo nazo zitakuwa na usanii sanii tu. Siyo serious. Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye anaweza wasikiliza Mawaziri hawa na kwenda kuchanja.

Wengi wakisikiliza Mawaziri hawa ndio wanakata tamaa kabisa ya kuchanja. Hawa walituaminisha Chanjo hizi hazifai. Ni biashara haiwezekani chanjo ikawa ndani ya mwaka mmoja. Leo watatuaminisha vipi zinafaa? Rais tuondolee hawa waigizaji.
 
Hamtafanikiwa na kampeni zenu za kupongeza wajingajinga kama askofu Gwajima. Amepata mtu ambaye anaweza kuwa na drama kama yeye! na sasa Gwajima anapata shida maana anataka yeye pekee ndiye awe drama king.

Waziri wa Afya hajafanya kitu chochote kibaya sasa kuna sababu gani ya kumtoa tena kwa kuongea ukweli!. Rais anatakiwa aache kusikiliza watu kama wewe wanaopenda drama za kijinga wakati watu wanakufa
 
Aise kuna watu bado wanasikiliza masalia ya mwendazake?

Mimi binafsi sifati ushauri wowote wa hio Wizara mana kwanza waliopewa dhamana wamepiga Uturn hatari sana ntachanja kujilinda Na pia ni msomaji mzuri wa vitabu Hivo naelewa umuhimu wa Chanjo

Na naungana Na Rais Samia kusema Science ni bora zaidi ya Jadi, Shida hawa wataalamu wetu wa Wizara ni masalia ya mwendazake fukuza wote Rais, Mtu anasema kuwa huyu alicheza ngono sijui shemeji what for? For national interest tena msemaji amebeba dhamana kubwa haswa
 
Waliosema Corona haipo Tanzania ni:
Magufuli
Samia
Mawaziri wote
Wachungaji kasoro RC tu
Masheikh
Wadanganyika a.k.a Watanganyika.

Lawama ziende kwa wote wakiongozwa na Kinjekitile Magu.
 
Waliondoa hadi Mloganzila kuwa University teaching hospital , mawazo mfu kabisa.
 
Huyo unayemuandikia naye alikuwa bosi wao (VP) ndani ya timu. Msimamo wao ulikuwa mmoja: Tanzania hatuhitaji chanjo. Hiyo moral high ground ya kuwawajibisha hao comedians wa wizara ya afya anaipata wapi?
 
Samia ndie mama wa hilo tatizo, usilaumu tawi la tatizo, laumu mizizi ya tatizo.

Samia pia ndie mwenyekiti wa CCM,
 
You aren’t serious. Kwanini unahangaika na peripherals? Au unatafuta kondoo wa kafara? Hujui kuwa mnafiki number one hapo ni Samia mwenyewe? Hao wote ni uzao wa panya! Otherwise, no one should compromise when matters of principle are at stake!

Thomas Jefferson, a former U.S. president, once said:

“In matters of principle, stand like a rock; in matters of taste, swim with the current. ”

Kati yao hao wote (Cabinet nzima), who stood like a rock one year or so ago?
 
Kama ni chanjo hata walete nani sidhani kama watu watachanja...hizo chanjo wanazodai wanataka kuagiza mil 17 watamchanja nani? Chanjo ni hiari sio suala la kufanyia propaganda. Hata aje nani sidhani kama watu watajitokeza kuchanja..

It's unfortunate baadhi ya watu wanaona wasiochanja kama vile wao hawana akili...hata hao watu mnao wadharau wa kijijini they can smell the danger. Walio chanja wachanje., tusiotaka tuachwe. Hatutaki haya makelele kila siku inachosha.
 
Huyu mama hafai kushika wizara nyeti Kama hiyo,akiimaliza hii awamu akiwa waziri wa afya ashukuru Mungu,sioni future nzuri kwa huyu mama tangu enzi za Magufuli,asipobadilika huyu mama ataishia pabaya.

Huyu mama naona Kama hawaendani na mama Samia,
 
Huyu mama hafai kushika wizara nyeti Kama hiyo,akiimaliza hii awamu akiwa waziri wa afya ashukuru Mungu,sioni future nzuri kwa huyu mama tangu enzi za Magufuli,asipobadilika huyu mama ataishia pabaya.

Huyu mama naona Kama hawaendani na mama Samia,

All you need to get along with any African leader is hypocrisy!
 
Hivi kwa niniwatanzania wanapenda mtu goi goi . Tumepata chapakazi mnaanza kumletea majungu!
 
Enzi zile hii Wizara iliendeshwa kwa weledi mkubwa sana na Mh. Dr Hussein Mwinyi, ambaye kwa sasa ni Rais wa SMZ.

At least Dr. Abel Makubi anajitahidi kadri ya uwezo na vile alivyojaaliwa.
 
Hamtafanikiwa na kampeni zenu za kupongeza wajingajinga kama askofu Gwajima. Amepata mtu ambaye anaweza kuwa na drama kama yeye! na sasa Gwajima anapata shida maana anataka yeye pekee ndiye awe drama king. Waziri wa Afya hajafanya kitu chochote kibaya sasa kuna sababu gani ya kumtoa tena kwa kuongea ukweli!. Rais anatakiwa aache kusikiliza watu kama wewe wanaopenda drama za kijinga wakati watu wanakufa
Alichoandika mtoa mada ni kweli. Compare ummy mwalimu na dorothy gwajima.
Waziri wa Sasa wa afya achilia mbali kuelewa vyema wizara anayoisimamia yawezekana hata yeye mwenyewe hajielewi.

Nafahamu vyema mheshimiwa Rais anamwona na anajitahidi kumpa muda arekebishe utendaji kazi wake. Haiwezekani wakati taifa linapitia changamoto ya covid-19, waziri yupo anapeana mipasho na shemeji yake.

Mpaka Sasa waziri gwajima hajaweka mikakati yoyote ya kutoa elimu juu ya chanjo kuondoa hii dhana potofu iliyoko kwa wananchi.

Pia waziri akumbuke alikuwa miongoni mwa wapinga chanjo enzi za jpm(watanzania sio wajinga).

Mama Samia. Ondoa Huyu waziri wa afya na naibu wake. Ni kituko katika wizara hii.
Watanzania sio wajinga.
 
Back
Top Bottom