Pre GE2025 Rais Samia: Tusikubali kugawanywa kwa sababu za kisiasa

Pre GE2025 Rais Samia: Tusikubali kugawanywa kwa sababu za kisiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi Watanzania kuwakataa wale wote wanaotaka kuligawa Taifa kwa sababu za kisiasa au tofauti za kiitikadi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Ameyasema hayo katika kilele cha Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa lililofanyika katika Uwanja wa Majimaji Songea, mkoani Ruvuma ambapo amewasisitiza Watanzania kutanguliza maslahi ya nchi kabla ya kutanguliza maslahi binafsi, pamoja na kutunza maadili na utamaduni wa Kitanzania.

Samia amewasisitiza Watanzania kuwa ni wamoja, wenye nia moja, hivyo hawana sababu ya kutofautiana.

"Niwaombe Watanzania tuwakatae wanaotaka kutugawa kwa sababu za kisiasa au tofauti za kiitikadi. Watanzania ni wamoja nia yetu ni moja sisi ni mtu mmoja," amesema.

Soma pia: Hotuba ya Rais Samia Septemba 17, 2024, ni hotuba ya kupongezwa na yenye mamlaka itapendeza mafisadi wafikiwe pia

Sambamba na hilo, ameeleza juu ya uwepo wa changamoto ya mmomonyoko wa maadili, akiitaka Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kulikabili hilo.

"Kutokana na mwingiliano wa tamaduni kutoka nje tumeanza kushuhudia mmomonyoko wa maadili na vitendo visivyofanana na Utanzania," amesema.

Kauli ya Rais Samia inakuja siku muda mchache tangu CHADEMA kufanya maandamano ya kushinikiza uchunguzi wa utekaji unaoendelea nchini.

 
Back
Top Bottom