Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewasihi Watanzania kuwakataa wale wote wanaotaka kuligawa Taifa kwa sababu za kisiasa au tofauti za kiitikadi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Ameyasema hayo katika kilele cha Tamasha la Tatu la Utamaduni la Kitaifa lililofanyika katika Uwanja wa Majimaji Songea, mkoani Ruvuma ambapo amewasisitiza Watanzania kutanguliza maslahi ya nchi kabla ya kutanguliza maslahi binafsi, pamoja na kutunza maadili na utamaduni wa Kitanzania.
Samia amewasisitiza Watanzania kuwa ni wamoja, wenye nia moja, hivyo hawana sababu ya kutofautiana.
"Niwaombe Watanzania tuwakatae wanaotaka kutugawa kwa sababu za kisiasa au tofauti za kiitikadi. Watanzania ni wamoja nia yetu ni moja sisi ni mtu mmoja," amesema.