Rais Samia: Tutaendeleza yale mazuri ya awamu ya 5

Rais Samia: Tutaendeleza yale mazuri ya awamu ya 5

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Rais Mama Samia akihutubia Taifa ktk kongamano la kidini jijini Dodoma, amesema ataendeleza mazuri tu yaliyofanywa awamu ya 5. Sijui wale wapiga mapambio mpo?

Akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa ataboresha haki, amani na demokrasia.

Wewe unayezuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani ole wako.
 
Ni mapema sana..........baada ya miaka kadhaa watu wasije wakaanza kuimba nyimbo nyingine..............CCM ni ile ile daima....zidumu fikra za mwenyekiti
 
Kuna watu hasa makada wa chama tawala sijui kwa nini hukwazwa sana na maneno "KUIMARISHWA KWA HAKI, USAWA & DEMOKRASIA". Bila shaka wamezoea vya kunyonga kwa hiyo basi vya kuchinja inakuwa ni mtihani mgumu sana kwao.
 
Pia amesema yeye na JPM ni kitu kimoja akimaanisha tuache kelele za kulinganisha kitu kimoja. Wote ni ccm, wanaongozwa na katiba ya ccm.
Yuko sahihi! Hata mimi ningekua katika nafasi yake, ningesema hivyo hivyo! Lakini mwisho wa siku nisingekubali hata kidogo wachumia tumbo kunigeuza kuwa mungu mtu wao, na pia kuiendesha nchi kwa kutumia mfumo hovyo wa kidikteta na usio thamini kabisa haki za kiraia kama alivyo fanya mpita njia!
 
Yuko sahihi! Hata mimi ningekua katika nafasi yake, ningesema hivyo hivyo! Lakini mwisho wa siku nisingekubali hata kidogo wachumia tumbo kunigeuza kuwa mungu mtu wao, na pia kuiendesha nchi kwa kutumia mfumo hovyo kidikteta na usio thamini kabisa haki za kiraia kama alivyo fanya mpita njia!
Anachomaanisha SSH ni kuwa JPM na yeye ni ccm, walinganishwe kimfumo na si kuwalinganisha kama watu.

Kimfumo wale ni kitu kimoja ila ni binadamu wawili tofauti.
 
Anasema kuwa awamu yake haijapigiwa kura wala kutokana na chama chengine cha siasa zaidi ya ccm? Hivyo hili neno awamu ni kutofautisha aliepita na sasa ila mambo ni yaleyale.
 
Mama Samia akihutubia Taifa ktk kongamano la kidini jijini Dodoma, amesema ataendeleza mazuri tu yaliyofanywa awamu ya 5. Sijui wale wapiga mapambio mpo?..
Mh SSH rais ni kitu kimoja na mwendazake ila sio sawasawa na mwendazake. So wapambe wa mwendazake mlijue hilo
 
Pia amesema yeye na JPM ni kitu kimoja akimaanisha tuache kelele za kulinganisha kitu kimoja. Wote ni ccm, wanaongozwa na katiba ya ccm.
Naona mleta UZI kajisahulisha kuhusu hii kauli kachagua yaliyompendeza tu.
 
Pia amesema yeye na JPM ni kitu kimoja akimaanisha tuache kelele za kulinganisha kitu kimoja. Wote ni ccm, wanaongozwa na katiba ya ccm.
ndio, Katiba. yule jamaa hakufuata katiba, alikuwa yeye ndio katiba. Na pia mama ameunda tume ya watalamu kuhusu COVID ambayo jiwe alidai haipo, haidi ikamuua na yeye
 
Magufuli ni marehemu, naona bado hamuamini kama mungu wenu kafa,,
Ndio ni marehemu, pengine ameoza na mifupa sasa. Hilo nalifahamu.

Wewe unafahamu kuwa CCM ndiyo chama tawala?
 
ndio, Katiba. yule jamaa hakufuata katiba, alikuwa yeye ndio katiba. Na pia mama ameunda tume ya watalamu kuhusu COVID ambayo jiwe alidai haipo, haidi ikamuua na yeye
Nchi bado ipo mikononi mwa Ccm. Kama wewe ni mpinzani hilo kaa nalo kichwani.
 
Back
Top Bottom