Sio bahati mbaya rais Samia amekwenda Marekani wakati huu taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani likiwa katikati ya mtanange mkali wa uchaguzi. Na mara hii ni kati ya mhafidhina Donald Trump na mwanamama Kamala Harris.
Mtu hawezi kushindwa kufikiri kuwa kimya kimya rais Samia amekuwa kwenye kampeni za urais wa Marekani kwa kujua ama kwa kutojua. Hii ni mara ya pili rais Samia anakwenda Marekani ndani ya kipindi cha takriban mwaka mmoja hivi.
Wamarekani wakati huu wa uchaguzi wakimwona rais mwanamke tena kutoka nchi ya dunia ya tatu ambapo demokrasia ni majaaliwa tu basi wamarekani wanajisikia kuwa nyuma ki-demokrasia na jambo hili linaweza kuathiri maamuzi yao wakati wa upigaji kura.
Ama kweli siasa ni sayansi na ingekuwa tunafanya siasa zetu kisayansi tungekuwa mbali sana.
Swali ni je, rais Samia atarudi amejifunza nini kuhusu demokrasia na uchaguzi huru na wa haki? Je Samia ataguswa kujenga mazingira yanayoruhusu uchaguzi kufanyika chini ya tume huru ya uchaguzi? Je Samia atajifunza “fair play “ kwenye chaguzi zetu ambazo Tumeona wagombea wengi wakipitishwa bila kupingwa huku wapinzani wakienguliwa bila sababu za msingi?
Hiyo ndio zawadi tunayoisubiri kutoka kwa rais wetu mama Samia pindi arudipo kutoka ziarani Marekani na Cuba.