Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Kwa kweli inashangaza jinsi CCM ilivyogeuka na kuwa chama kisichojali habari za wananchi.
Inashangaza nchi hii ina Rais mwanamke, ina Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) ina jumuia ya wazazi lakini leo hii wote hao wanashindwa kutoa kauli kukemea kauli ya kifedhuli, ya kibaradhuli na ya kibri kikubwa sana ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa mama mjamzito anayehitaji kujifungua lakini hana uwezo.
Hebu tujiulize ingekuwa ni uwenyekiti wa Nyerere au CCM ya Nyerere, huyu mkuu wa mkoa wa Dar es salaam angeweza kutoa kauli ya kiburi namna hii.
Chalamila anamwambia mama mjamzito ambaye mi masikini kuwa kama huna hela kamwambie mumeo akupasue yeye mwenyewe kwa mkasi.
Maneno gani hayo!
Inakuwaje kwa Samia ambaye ni mwanamke, tena ni mama, answezaje kufumbia macho kauli kama hii?
Inakuwaje umoja wa eanaeake wa CCM na jumuia ya wazazi inafumbia macho kauli hii?
Tafsiri tunayoipata ni kuwa wote hao wanaunga mkono kauli ya Chalamila. Na ndiyo malipo yao kwa Watanzania.
Sikitiko kubwa lililoje nchini!