Rais Samia unanisikitisha sana; hukujifunza kwa Kikwete na hutaki kijifunza kwa Magufuli

Unataka mama awe dikteta kama Magufuli aanze kuuwa watu hovyo? Mbona haruhusu maandamano? Unafikiri Tanzania tuna demokrasia kuliko Malawi au Kenya? Je yanayoendelea Kenya na Odinga yanaweza kuruhusiwa Tanzania? Ruto anatukanwa majukwaani kuliko Samia. Acha kuingilia uhuru wa watu. Mbona mmezoea kutawaliwa kidikteta nyie? Anayoyafanya mama ingekuwa nchi nyingine angeshaondolewa madarakani kitambo.
 
NCHI imempwelepweta.

Ameshindwa.

Mwisho kuwapa wanawake.



M-judge Kama mtu na sio kama mwanamke.

Hata wanaume mbona huwa wanakosea?!

Kwani walotufikisha hapa tangu Uhuru zaidi ya miaka 50 hakuna uhakika wa huduma ya maji wala umeme ni kina nani Kama sio Viongozi wanaume?

Imagine Maji na umeme kama huduma za msingi kabisa uhakika wa kupatikana through out the year haupo?! [emoji848][emoji848]
 
Ninyi ndio mlikuwa mnasifu kwa nyimbo na mapambio huku mkiimba anaupiga mwingi leo kiko wapi?.Kila kona kilio
 
Thread of the year JF ndo hii
 
UZURI ANATAWALA TANZANIA.
HUKO TANGANYIKA A.K.A KUZIMU HAPAJUI.
 
Ubandidu bila matokeo chanya ni vita mzee! JPM na ubabe wake ila wananchi waliona matokeo chanya. Ufanye ubabe huku unauza nchi nani atakuelewa?
 
Exactly Hawa mbwa sio wakuwatendea wema kbs
 
Ikifika miezi ya robo Mwaka ya mwisho kila Mwaka kuanzia around mwezi September-December/Januari mvua za Vuli zisiponyesha za kutosha huduma ya Maji inakata kabisa na umeme kwa kila Mwaka .

Hayo hayakusabishwa na kiongozi mwanamke.

Sipati picha Mungu akiamua kubana Vuli isinyeshe Na kufuatiwa na mvua za Mwaka zisinyeshe Mwenyezi Mungu atuepushie mbali.

Viongozi wanaume Ndiyo wametufikisha kwenye hali ngumu matatizo, kero na changamoto zilizopo chungu nzima na sio Rais Samia sababu ya uanawake wake.

Ahukumiwe kwa haki ,

Akosolewe Kama mtu/binadamu wa kawaida bila kujali jinsia yake.

Asomaye na afahamu ujumbe huu.
 
Mlioko karibu na Rais Samia mpeni ushauri huu:

Kwamba aupige chini mkataba wa DP maana mwitikio wake kwenye jamii umekuwa hasi kwa kiasi kikubwa.

TPA waendelee kusimamia Kwa ufanisi na watanzania wanaweza. InshaAllah.

Ni wazi inaonesha kuna tatizo au matatizo bayana kwenye hilo.

Tafakali Mheshimiwa kisha chukua hatua.
 
Huu mwezi wa 7 bado miezi 2-3 hivi utaona nchi inaanza kuingia gizani sababu ya kukosekana Kwa huduma ya umeme,

Kukosekana Kwa huduma ya Maji,

Na sababu Umeme wetu hutegemea Maji hivyo kukosekana kwake huenda sambamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…