Rais Samia, unapoteua zingatia watumishi wa muda mrefu na wenye uzoefu serikalini badala ya kuwatoa mtaani

Kuna vyeo inategemea Rais ataamkaje siku hiyo, muda wowote you are out...
 
Mimi sina imani na huyu mama kabisa sijui kwanini..yaani hata afanye chochote naona kama boko tu.
Pengine utakuwa na unatawaliwa na chuki za kidini. Hakuna aliye mkamilifu lakini katika muda mfupi amejipambanua kuwa ni kiongozi mpenda haki na anayesikiliza wengine wanasema nini. Tumpe muda atafanya makubwa zaidi.
 
Hizo nafasi ni kwa makada wa CCM tu hata kama ni wahalifu wanakula shavu tu
 
Umeongea hoja ya maana mno!

Mamlaka za uteuzi zinatakiwa kuzingatia huu ushauri [emoji817]%
 
Kuchanganya kama ulivyosema ni sawa,lakini kumchukua PHD holder unaweka kwenye rank mmoja na muigizaji wa bongo movie kwa maoni yangu sio sahihi
By the way ni matakwa ya Mhe. Raisi kumteua yeyote anaeona atamsaidia, sawasawa ana Phd au hana.
 
Watumishi wa umma si walengwa kwa nafasi za RC, DC ila line ya utumishi wa umma inaruhusu uteuzi katika nafasi za ukatibu mkuu, DAS, DED na ukuu wa taasisi za umma. Tuendelee kuamini mama yetu Rais Samia atarudi kwenye misingi hiyo iliyotumika awamu ya kwanza hadi ya tatu. Kundi hili muhimu lisiachwe bila kulitumia ipasavyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…