Rais Samia, usiwasikilize sana washauri wako kuhusu Mkataba wa Bandari

Rais Samia, usiwasikilize sana washauri wako kuhusu Mkataba wa Bandari

Daisam

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2016
Posts
2,625
Reaction score
3,141
Mama, usiwasikilize sana washauri wako hasa kuhusu Mkataba wa DP World. Tumia akili yako wewe mwenyewe kutoa maamuzi ya mwisho kuhusu Mkataba wa DP World.

Kwa ufupi kabisa, na kwa maoni yangu, kuna kila sababu kuusitisha kwanza mkataba huu mpaka pale utakapokuwa umeeleweka vizuri kabisa kwa Watanzania wote wa makundi yote.

Hakuna mshauri wako hata mmoja atakayekwambia kuwa mkataba huu una mapungufu. Wote waliokuzunguka zaidi ya 90% wanaweza kuwa wanafiki tu.

Wanajali maslahi yao tu, si maslahi mapana ya Taifa.
Tumia mamlaka yako kama Mkuu wa Nchi kusitisha kwanza kwa muda mkataba huu.
 
Huo mkataba ulisha kamilika na kusainiwa kelele za chura hazizuii ngombe kunywa maji, watanzania wengi ni wanafiki hawatakuelewa huo sio mkataba wakwaza, sema tu ni wakwanza kuwekwa hadharani, na yote ingekua inaletwa hamna hata moja utakao kubalika ni hi jamii yetu ulio jaa wanafiki.
 
Ndugu yangu unapoteza muda wako bure kushauri wapumbavu[emoji53][emoji53][emoji53][emoji53][emoji53]
 
Rekebisheni vifungu vyenye utata ambavyo watanzania wanavipigia kelele!! Acheni ujinga wa kufikir kila mpingaji wa vifungu ni mwizi!!
Sasa si mmeshaambiwa mikataba bado haijasainiwa na maoni yenu yamesikilizwa mnaendelea kupiga kelele za nini au mnadhani mnaongea na viziwi?
 
Wapigaji bandarini hawataki ibinafsishwe waendelee kuiba
Sababu ya kitoto hiyo. Kama kuna uzembe wa usimamizi wa sheria taratibu na kanuni za kulinda rasimali za Taifa, mamlaka za uteuzi ziwashughulikie wateule wao
 
Sasa si mmeshaambiwa mikataba bado haijasainiwa na maoni yenu yamesikilizwa mnaendelea kupiga kelele za nini au mnadhani mnaongea na viziwi?
Mkataba umepelekwa Bungeni, baada ya kuvujishwa, tayari umekwisha kusainiwa na pande zote. Na kwa kuwa Bunge limeridhia, hakuna cha zaidi ila kuambatinisha maridhio hayo ya Bunge
 
Sababu ya kitoto hiyo. Kama kuna uzembe wa usimamizi wa sheria taratibu na kanuni za kulinda rasimali za Taifa, mamlaka za uteuzi ziwashughulikie wateule wao
Tangu tumepata uhuru bandari imekua ni lango la upigaji .sasa Acha aje mwekezaji aweke mashine tuone hao wapigaji wataishi vipi. Uwezo wa kuoboresha bandari iwe ya kisasa kama ya dubai sisi hatuna tukubali tuu.
 
Mkataba umepelekwa Bungeni, baada ya kuvujishwa, tayari umekwisha kusainiwa na pande zote. Na kwa kuwa Bunge limeridhia, hakuna cha zaidi ila kuambatinisha maridhio hayo ya Bunge
Basi tulieni mletewe maendeleo.
 
Sasa si mmeshaambiwa mikataba bado haijasainiwa na maoni yenu yamesikilizwa mnaendelea kupiga kelele za nini au mnadhani mnaongea na viziwi?
Ile mikataba mibovu iliyopitishwa miaka ya nyuma na CCM masikio mliyapeleka mirembe ama? Watanzania na viongoz mbalimbali wa dini wanawajua nyie kuhusu mikataba ndio maan.. hawapoi kukosoa!!
 
Back
Top Bottom