BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ifikapo Januari 2024, kinu cha kwanza kati ya tisa vilivyopo katika bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kitawashwa na kuruhusu uzalishaji wa nishati hiyo kuanza.
Rais Samia amesema baada ya kuwashwa kinu cha kwanza, cha pili kitawashwa kabla ya Aprili 2024, hivyo kuongeza uzalishaji wa umeme.
Amesema hayo jana usiku Jumapili, Desemba 17, 2023 katika hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora (PMAYA). Pia amesema pamoja na jitihada nyingine uwashaji wa vinu hivyo vitakwenda kupunguza malalamiko la kukatika kwa umeme.
“Pamoja na jitihada nyingine za gesi, sola na mambo mengine, lakini katika umeme wa hydro (maji) tunategemea nadhani katikati ya mwakani malalamiko mengi yatakuwa yamepungua," amesema Rais Samia.
Pia amesema licha ya sekta ya viwanda kushuka duniani, bado Tanzania imesimama na kufanya vizuri. Kwa mujibu wa Ripoti ya Dunia ya 2024 ukuaji wa viwanda ulimwenguni umeshuka.
Amesema takwimu hizo zinaonyesha mambo mawili ambayo endapo kuna changamoto ya kushuka kwa viwanda, kuna haja ya Serikali kukaa na wenye viwanda ili kuzungumza kwa uwazi na kusema wanayoyaona na wao kupokea na kuyatekeleza.
Jambo la pili ni jitihada za Serikali, lazima kulenga katika utegemezi wa viwanda vya ndani kutumia malighafi kutoka nje na kutafuta mbadala wa malighafi hapa nchini au kuvutia uwekezaji zaidi wa malighafi inayotumika kwenye viwanda vingine.
"Nimeambiwa kuna kufanya ‘assembling’ ya magari kule Kigamboni, lakini vioo wanavyotumia vinazalishwa hapa Tanzania kule Mkuranga. Tukiwa na viwanda vingi vya namna hiyo vitatusaidia kupunguza gharama za kununua malighafi nje na kupunguza uzalishaji,"amesema Rais Samia.
Akizungumzia stempu za kielektroniki, amesema wapo kwenye mazungumzo na shirika linalotengeneza na kuna dalili kukubali kushusha gharama za stempu.
Shirika hilo ambalo limezungumziwa ni la Societe Industielle de Produits Alimentaire (SICPA) la Uswisi linaloendesha mradi wa stempu za kodi za kielektoniki.
Hata hivyo, Rais Samia amesema wanaangalia uwezekana na wameanza mazungumza na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watumie mfumo wa kielektroni, badala ya kusumbuana na mtu.
MWANANCHI
PIA SOMA
- Arab Contractors na Elsewedy Electric Kukabidhiwa Rasmi Eneo la Rufiji (PHPP) Kesho
- Arab Contractors wakabidhiwa Billion 688.6 kama malipo ya awali mradi wa umeme wa maporomoko ya mto Rufiji
- Serikali Yakabidhi Eneo La Mradi Wa Umeme Wa Maji Mto Rufiji Kwa Mkandarasi Tayari Kwa Kazi Kuanza
- Rais Magufuli kuzindua mradi wa umeme Mto Rufiji Julai 26, 2019
- SADC yamuunga mkono Rais Dkt Magufuli ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme Rufiji
- Uzinduzi Mradi wa Umeme, mto Rufiji: Rais Magufuli aagiza sehemu ya Selous kuwa Hifadhi ya Taifa
- Mbunge Sospiere Mukweli ameniogopesha kwa kauli yake kuhusu ujenzi wa bwawa la Rufiji; je, kuna haja ya wabunge wote kupimwa akili?
- Mradi wa Kufua Umeme Rufiji (MW 2115) uchimbaji kina cha lango la kuingilia maji kwenye mitambo wakamilika
- Kampuni ya ElSewedy Electric Co inayotengeneza bwawa la umeme Rufiji imewekewa vikwazo, haitaweza kukopesheka nje
- Waziri Makamba: Msitegemee wala kutarajia bwawa la mto Rufiji kujazwa maji mwezi Machi
- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya mradi wa umeme wa mto Rufiji
- Dkt. Mpango: Mkandarasi wa Bwawa la Nyerere Hana Uzoefu, pia mradi upo nyuma ya muda
- Waziri Makamba: Ujenzi wa tuta kwenye bwawa la mwl Nyerere umekamilika
- Maji katika bwawa la Nyerere kuanza kujazwa 15/11/2021 na 13/04/2022 litakuwa limejaa tayari kwa majaribio
- PM Majaliwa: Bwawa la umeme kukamilika Juni 2022
- Tanesco:- Bwawa la Nyerere litakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 2115 hata kama mvua haijanyesha kwa miaka 2
- Waziri Kalemani: Bwawa la Nyerere kujazwa Maji Novemba 15, 2021. Umeme wa maji ni nafuu kuliko wa vyanzo vingine
- Kutokukamilika kwa Mradi wa Umeme Rufiji mwaka 2022 kama ilivyotakiwa na sasa Kukamilika 2024 ni Kumtukana na Kumdhalilisha Hayati Dkt. Magufuli
- Rais Samia kuzindua zoezi la ujazaji maji katika Bwawa la Julius Nyerere, Disemba 22
- Makamba: Ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere umefikia asilimia 67
- Makamba: Sisi tumeamua kuwa wakweli, bwawa la Nyerere linaisha Juni 2024. Adai tarehe ya mwanzo isingewezekana kwa namna yoyote
- Makamba: Itachukua misimu miwili ya mvua kujaza Bwawa la Nyerere
- Maji yatakayojazwa Bwawa la Nyerere (JNHPP) yanaweza kuzalisha Umeme kwa mwaka mmoja bila kutegemea mvua
- Rais Samia akishiriki shughuli ya kuanza kujaza maji Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), 22/12/2022
- TANESCO: Bwawa la Nyerere halitapunguza bei ya umeme
- Serikali: Mashine ya kwanza ya Kufua Umeme Bwawa la Nyerere itawashwa Mwezi Februari 2024
- Rais Samia: Uzalishaji Umeme Bwawa la Nyerere kuanza Januari 2024
- TANESCO: Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kuhusishwa na athari za mafuriko ya Kibiti na Rufiji ni kupotosha Umma
- Kamati ya Bunge: Bwawa la Nyerere litakamilika Juni 2024, Tsh. Trilioni 5.85 zimelipwa tayari
- Biteko: Shida ya umeme sasa basi, megawati 235 zimeingia Grid ya Taifa
- Rais Samia: Suluhu ya Umeme itapatikana Aprili 2024 baada ya kuanza uzalishaji wa Megawatt 470-500 katika Bwawa la Mwalimu Nyerere!
- Dotto Biteko: Tumezima mtambo wa bwawa la Mwl Nyerere
- TANESCO: Bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) kuhusishwa na athari za mafuriko ya Kibiti na Rufiji ni kupotosha Umma
- Profesa Tibaijuka: Mafuriko ya Rufiji hayajasababishwa na Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ila limeshindwa kuregulate mafuriko!
- Mtambo wa pili bwawa la Nyerere kuwashwa, kumaliza kabisa mgao wa umeme nchini
TUHUMA ZA UFISADI NA HUJUMA
- Mtaalam: Watanzania mnadanganywa Stiglers Gorge haiwezekani kwani Kina cha Maji Mto Rufiji kinapungua mno
- Hatma ya mradi Stiegler’s Gorge: Hatakama hatukubaliana kiitikadi, tukubaliane katika Ushauri wa kitaalam
- Hotuba ya bajeti Nishati; Miradi ya Rufiji na gesi itaumiza nchi: Mnyika aonya
- Tuambiwe ukweli: Stiglers Gorge inaweza kuwa maafa makubwa kwa taifa badala ya furaha
- Lissu: Serikali na benki hazina uwezo wa kujenga bwawa la Umeme Rufiji
- CAG: Bwawa la Nyerere liliharakiswa
- Polepole: Bwawa la Nyerere ni mradi wa kufa na kupona hatutakubali wahuni wauchezee, Winchi ni kitu kidogo sana!
- Inaumiza sana kuona mradi wa bwawa la Nyerere unahujumiwa wazi wazi
- Unakataje miti milioni 4 ili kujenga la umeme (JNHPP)
- Makamba: Mradi wa JNHPP upo nyuma kwa siku 477 (yaani mwaka na zaidi ya siku 100)
- UFISADI: Mpina aibua tuhuma za upigaji wa Sh. Trilioni 1.5 Bwawa la Nyerere
HISTORIA
- Mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere katika maporomoko ya mto rufiji unaotekelezwa na Serikali uliasisiwa na Baba wa Taifa mwaka 1975
- CAG: Mradi wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unatumia upembuzi wa mwaka 1970
- Mhandisi Mkazi, Upembuzi yakinifu wa 1980 unatumika bwawa la JNHPP
- Mwalimu Nyerere aliomba fedha Mradi wa Bwawa la Umeme Rufiji