GE2025 Rais Samia: Vijana walioandamana wametoka nje ya Tanzania

GE2025 Rais Samia: Vijana walioandamana wametoka nje ya Tanzania

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
dawa ni kula nao sahani moja pamoja na wale wate walio husika kuwapa hifadhi kwa namna moja au nyingine
 
"Tumesikitishwa na kuhuzunishwa na matukio ya uvunjifu wa amani, upotevu wa maisha na uharibifu wa mali za umma na mali za watu binafsi. Kilichotokea hakiendani na taswira na sifa za kitanzania na sio Utanzania. Haikutushangaza kuona kuwa baadhi ya vijana waliokamatwa kutokana na tabia hiyo, wametoka nje ya Tanzania.

Vyombo vyetu vya Ulinzi vya Tanzania vinaendelea kufuatilia na kuchunguza wa undani zaidi kilichotokea na kuirudisha nchi katika hali tulioiozea haraka." Rais Samia Suluhu Hassan.
View attachment 3496683
Kila wakati ni kujiliwaza tu kwamba watanzania hawezi kuchukua action kwa jambo linalowakereketa. Huko ni kuwakosea adabu watanzania, ni dharau za wazi. Msijifiche kwenye migongo ya watu wa nchi jirani. Watanzania sio maiti kama mnavyotaka ieleweke, wanafikiri pia. Hiyo action walioichukua ni wao wenyewe. Acheni kuwasingizia majirani.
 
Haya mambo huwa yanazunguka mpaka yanakufika Mungu wetu huwa analipa taratibu
Yatakuja kuwafika na familia zenu sijui mtakuja kusemaje
 
"Tumesikitishwa na kuhuzunishwa na matukio ya uvunjifu wa amani, upotevu wa maisha na uharibifu wa mali za umma na mali za watu binafsi. Kilichotokea hakiendani na taswira na sifa za kitanzania na sio Utanzania. Haikutushangaza kuona kuwa baadhi ya vijana waliokamatwa kutokana na tabia hiyo, wametoka nje ya Tanzania.

Vyombo vyetu vya Ulinzi vya Tanzania vinaendelea kufuatilia na kuchunguza wa undani zaidi kilichotokea na kuirudisha nchi katika hali tulioiozea haraka." Rais Samia Suluhu Hassan.
View attachment 3496683
Acheni kujifanya hamnazo, hata Sisi weusi tulivyokuwa tunataka kutoa Mkoloni, tuliambiwa kuwa ni wahuni, tumekodishwa, na blah blah zingine. Sasa hivi tuna wakoloni weusi tabia ni Ile Ile , wanataka Haki kuwa ni wahuni
 
Kwa hiyo wewe kudai umeshinda kwa kwa asilimia 97.6 wakati kila mtu anajua kuwa ni uongo, ndo Utanzania huo?

Are you dumb?
Na kama ni kweli hivyo asemavyo, yaani vijana toka nje waingie nchini ni kuviteka vituo vya polisi nakuvipiga viberiti. Nani aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu aliyepaswa kulinda mipaka ya nchi?? Kama ameshindwa kuwalinda Watz ni wazi kuwa hicho kiti kimeshampwaya mapema tu.
 
Ukifanya ubaya na ww nafsini unajua umefanya ubaya lakini bado unashupaza shingo ...Hua tunakuacha ....Kuna siku ytalipwa kwa maovu yako ww na kizazi chako..
 
Back
Top Bottom