Rais Samia: Vya bure hakuna, tozo daraja la Kigamboni zitaendelea na nyingine za barabara zinakuja

Rais Samia: Vya bure hakuna, tozo daraja la Kigamboni zitaendelea na nyingine za barabara zinakuja

Boss mkuu tuhurumie mbona awamu yako tulikupa kura kama zoooteeee
 
Kaongeza kwa Kusema
" Watu wanauliza kwanini Kigamboni tulipe wakati Tanzanite twapita bure?, "
Akajibu
" Kigamboni ni mkopo, Tanzanite sio mkopo ni mali ya serikali"

Akaongezea

" B...U...R....E havipo, hivyo wananchi wajizoeshe kulipia, na huko mbeleni mambo yote yatalipiwa kuanzia barabara na madaraja"....

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni alifumba macho,

Mbunge aliishia kucheka tu
Halafu Chadema wanamsengenya Shujaa Maguful

Tanzanite bure
 
Hakunaga Kura Za bure mkuu.
Hii iwe ni kauli mbinu ya mwaka 2025
Wao wanatembelea m v8 kwa kua tuliwaamini watupunguzie kero sana wanajibu jeuri kwa tozo zetu ..maji wameyachupusha town kivuko tulipe darajani tulipe kigamboni si wanatuona mafara fulani...
 
Habari zenu wadau..

Kwa Mujibu wa gazeti la Raia Mwema limeripoti kwamba Rais Samia amewataka Wananchi Wazoee Tozo kwani Tozo nyingine nyinginzinakuja kwenye Barabara..

Aidha Mbunge wa Gairo Ahmed Shabiby aliitaka Serikali kujenga Barabara kwa kushirikiana na sekta binafsi ambazo zitakuwa na kigezo Cha Tozo ndani yake.

Hii ilikuja baada ya Mbunge wa Kigamboni kumuomba Rais Kufuta Tozo za daraja la Kigamboni.
Ikumbukwe Serikali imeamua kuja na model ya kujenga Barabara kwa njia ya ubia na sekta binafsi na hivyo kuwa na component ya Tozo ndani yake..

Kazi iendelee 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20221109-142751.png
    Screenshot_20221109-142751.png
    174.8 KB · Views: 4
  • 20221112_103622.jpg
    20221112_103622.jpg
    179.3 KB · Views: 4
Hapo serikali inakosea hii mifumo, ya kibepari inahitaji nchi inayojiweza kiuchumi, kuwa na wazalishaji wengi ambao hawataona shida kulipa hizo tozo.

Lakini kwa tz ambapo watu wengi hawana huakika na kesho yao, halafu unawawekea tozo kila sehemu, unawarudisha nyuma kimaendeleo.
 
Wanataka kusema hela waliyotumia kujenga daraja la kigamboni haijarudi..pale kuna gharama Gani ya uendeshaji zaidi ya kuchukua fedha..wawe wa kweli kwamba wanataka wawapokonye nssf mradi wajikabidhi wao wapige hela..
Hawa watu Wana roho za ajabu sana.mwendo Kasi umejengwa kwa hela zetu..kisha unapewa kampuni binafsi wajichotee hela..hatujawahi patiwa financial report za mradi hadi leo...
Acheni wizi..daraja kibaki nssf maana ndio mradi pekee unaowaingizia hela za uhakika...hizo ni hela za wazee wetu
 
Kwa hiyo barabara zitakazojengwa zitakuwa si mali ya serikali?kweli kuuzwa kunakuja!
 
Mh Rais akijibu ombi la Wabunge wa Kigamboni kuhusu kuondoa tozo za daraja, amesema kuwa lile daraja lilijengwa kwa mkopo hivyo lazima watu walipe hela kupita, vya bure havitakuwepo, hivyo wananchi wategemee kuanza lipia barabara watumiazo, zitazojengwa na ppp.

Kivuko cha Kigamboni kubinafsishwa ili kuondolea Serikali gharama za uendeshaji
Vya bure HAKUNA, lakini juzi tumeambiwa China imetusamehe madeni yetu yote na wanataka tupeleke mazao yetu bure...
 
Tatizo watu wanakosea wanapoipa serikali umuhimu wasio nao.

Utasikia Mh rais,

Hongera mheshimiwa rais

Mh rais tunaomba hiki, ujinga ujinga tu.

Wapuuzeni hao mafisadi, jali familia yako, wanajamii wenzako na endelea kupambana upate pesa.

Hawa serikali msiende hata kwenye event au jambo lolote wanalafanya.

Msiwape umuhimu.
Point...mm ndiyo naishi kwa mfumo huo

Ova
 
Mh Rais akijibu ombi la Wabunge wa Kigamboni kuhusu kuondoa tozo za daraja, amesema kuwa lile daraja lilijengwa kwa mkopo hivyo lazima watu walipe hela kupita, vya bure havitakuwepo, hivyo wananchi wategemee kuanza lipia barabara watumiazo, zitazojengwa na ppp.

Kivuko cha Kigamboni kubinafsishwa ili kuondolea Serikali gharama za uendeshaji
Hivi ni ccm=umasikini Mshawai jiuliza daraja la cramia lenye urefu wa kutoka Dar hadi zanziber baharini lilijengwa kwa bei gani,lina km ngapi linanjia ngapi watu wanapita bure.

Hili lakwetu hata km 1 haifiki limejengwa pesanyangi sana kuzidi hata hili la cramia kwsabu ya upigaji bado mnatwisha mzigo raia utafikiri kigamboni sio sehemu ya Tanganyika.
 
Tatizo watu wanakosea wanapoipa serikali umuhimu wasio nao.

Utasikia Mh rais,

Hongera mheshimiwa rais

Mh rais tunaomba hiki, ujinga ujinga tu.

Wapuuzeni hao mafisadi, jali familia yako, wanajamii wenzako na endelea kupambana upate pesa.

Hawa serikali msiende hata kwenye event au jambo lolote wanalafanya.

Msiwape umuhimu.
Umeongea point kila kitu rais
Wakat kuna maDC,RC,maded, PM wanafanya vizur tu lakin hawapongezwi inafanya viongoz wajionea siyo lolote.
 
Back
Top Bottom