Rais Samia, wakulima wa Miwa wanatishia kukibomoa Kiwanda cha Sukari cha Mbigiri

Hapa mkulima anakosa gani mpaka anaongezewa riba ya adhabu!?

Hakuna namna serikali iwajibike kuwanusuru wakulima hawa wanyonge baada ya ulaghai au kutokujali madhara ya maamuzi ya serikali kuwashawishi wakulima waingie ktk kilimo hiki cha miwa halafu wakaingia hasara kisha kuwatupa bila fidia au kulipwa Jasho lao.
 
Wa kumlaumu hapa ni William Erio aliyemfitini aliyekua DG wa nssf wakati wa 2016-18 ambaye aliondolewa wakati anapambana kujenga viwanda vya mbigiri na mkulazi.
Baada ya kumfitini na kumuondoa na yeye kuridhi mikoba yake, hakufanya chochote ktk miradi hyo na hivyo kupelekea haya kutokea

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Fitna ya Erio ndo imeleta matatizo yote haya

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Akamatwe Erio aeleze nini kimetokea viwanda haviendelei

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Kutoka mbigiri hadi mtibwa kuna umbali gani?
 
Anapaswa kuubeba mzigo huu.
Kasababisha umasikini wa kutupwa kwa wakulima wasio na hatia yoyote.
 
Kutoka mbigiri hadi mtibwa kuna umbali gani?
About 50km.
Lakini kutaka kufaham umbali kutoka Mbigiri mpaka Mtibwa ni sawa na kupalaumu ulipoangukia na kupaacha ulipojikwaa.
Watu wanataka kufahamu hapa walipojikwaa kuna nini.
 
Serikali ijiepushe kufanya biashara kama hizi. Kuna risks nyingi sana. Na kwasababu ya kukosa weledi, hasara zinaweza kuleta shida mbele ya safari
Na serikali inapoamua kuacha kabisa kuwekeza kwa/ au kufanya biashara na private sector, kila mtu analalamika
 
Na serikali inapoamua kuacha kabisa kuwekeza kwa/ au kufanya biashara na private sector, kila mtu analalamika

Biashara kama reli au ndege ni sahihi kabisa kwa serikali. Ila mabasi wawaachie wakinga. Kuanza vituo vya kuuza mafuta wawaachie kina mangi
 
Na serikali inapoamua kuacha kabisa kuwekeza kwa/ au kufanya biashara na private sector, kila mtu analalamika
Unamaanisha nini!
Serikali kazi yake ni kusimamia sekta binafsi na yenyewe inatakiwa kukusanya kodi na siyo kufanya biashara.
 


Sasa kukibomoa kiwanda itasaidia nini kama sio kuendeleza ujinga na umasikini. Yaani serikali inajaribu kuwaletea kiwanda halafu wakibomoe. Watanzania wana utamaduni wa kulalamika huwezi kupata serikali inafanyia watu vitu vingi kama watanzania wakulima halafu ni walalamishi kila siku kuna viongozi kibao lakini utakuta hata habari hizi wakulima hao hawajawaambia kuna wabunge......... wako wapi?. Mkitaka kujua Tanzania tuna wavivu wengi tuwaruhusu wakenya waje kulima Morogoro kwa miaka 5 tu tuone.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…