Jana katika hafla ya kuipongeza timu ya Yanga ikulu Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu ametegua siri ya mapenzi na ushabiki wa timu anayoishabikia Rais wa TFF Walace Karia.
Kwa muda mrefu Karia amekuwa akihusishwa na mapenzi ya lia lia na timu ya Simba lakini mwenyewe amekuwa akidai yeye ni shabiki wa timu ya Coastal Union ya Tanga.
Wakati Rais anazungumza alisema alimuuliza Naibu Waziri Mwinjuma kwamba Karia ni timu gani? Akajibu ni Coastal.
Lakini Rais Samia akaweka wazi kwamba Karia ni Simba kama ilivyo kwa Naibu huyo.
Kwa muda mrefu Karia amekuwa akilalamikiwa kuegemea upande wa timu fulani kwa sababu ya mapenzi makubwa ya timu hiyo aliyokuwa nayo.
Hakuna kiongozi anayeongoza mpira akakosa kuwa mpenzi wa timu fulani, kinacholalamikiwa ni kuendekeza mapenzi kiasi cha kufanya upendeleo dhidi ya timu usiyoishabikia hali ya kuwa ni kiongozi unayesimamia mpira.
Rais ameshasema wewe ni nani upinge.