Hii mbinu Huwa inatumika maeneo mengi sana sio tuu Kwa wakwepa.kodi Bali Hadi Kwa Polisi wanaotaka Kukamata Baadhi ya watu au kuzuia jambo Fulani.
Sasa Leo Mkuu wa Nchi amekataa kutoa kibali Cha maelekezo kutoka Juu kwamba ni janja janja ya watu wachache kukwepa kuwajibika.
Swali:
Je Wananchi waanze kukaidi Kauli za maelekezo kutoka Juu?
======
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameelezea kukerwa na matumizi ya kauli ya “maelekezo kutoka juu” kama kisingizio cha kukwepa kodi na kufafanua kuwa hajawahi kutoa maagizo kama hayo.
Akizungumza Alhamisi, Januari 23, 2025, katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa walipa kodi bora wa mwaka 2023/2024, iliyofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kila mfanyabiashara kulipa kodi bila upendeleo.
“Mimi sijawahi kutoa maelekezo mtu asilipe kodi, na ikitokea haja ya kufanya hivyo, shirika au mtu asilipe kodi, nitafanya kwa maandishi na sio mtu aje kwa mdomo. Maelekezo kutoka juu, mimi sijawahi kufanya hivyo,” amesema Rais Samia, akihimiza uwajibikaji wa kodi.
Aidha, Rais Samia ameeleza kuwa ukwepaji kodi unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara unaondoa usawa katika biashara na kuwaumiza wale wanaofuata sheria kwa kulipa kodi.
Rais ametoa wito kwa watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha usimamizi wa haki katika ulipaji kodi na kuhakikisha kila mfanyabiashara anachangia maendeleo ya taifa kwa kufuata taratibu zilizopo
View attachment 3212279