Rais Samia Watalii na Uwekezaji unaojivunia hautakuwepo kama Usalama wa nchi ni wa kusuasua. Vijembe havisadii unazidi kubomoa

Rais Samia Watalii na Uwekezaji unaojivunia hautakuwepo kama Usalama wa nchi ni wa kusuasua. Vijembe havisadii unazidi kubomoa

Wakuu,

Katika Mkutano leo Rais Samia amejitapa kuwa nchi ipo salama, lakini pia utalii na uwekezaji unaongezeka. Kwa matukio yanayoendelea ni kweli kuna usalama? Wewe jibu unalo lakini pia watanzania majibu wanayo.

Mnapoingia chaka ni kudhani matukio haya yanaathiri tu wananchi wa wachache, mnashindwa kuangalia kwenye picha kubwa kuwa matukio haya ya kutisha hayaishii tu Tanzania, Dunia inaangalia na kujua kinachoendelea, hii siyo nzuri kwenye uwekezaji na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Pia soma: Rais Samia Kwa Mabalozi: Hatupo hapa kuelekezwa nini cha kufanya kwenye nchi yetu

Hakuna mtu atajihisi salama kwenda kuwekeza kwenye nchi ambayo muda wowote anaweza kutekwa na kuuliwa, wala kwenda kutalii kwenye mazingira kama haya.

Hizo nchi unazotoa mifano watoto kwenda bastola shuleni, sijui wapi mtu kaua kundi la watu, wote wahusika wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki ama wanauliwa on the spot. Huwezi kulinganisha na hapa ambako watu wanatekwa back to back na hakuna yoyote anayewajibishwa kwenye haya. Si kwa viongozi kujiuzulu wala kwa wahusika wa vitendo hivi kukamatwa.

Kwa mazingira kama haya unategemea wananchi watakaa kimya?

Badala ya kutoa vijembe na kuchamba wanaohamaki na wanaokosoa hatua za konono kutoka kwenye vyombo vya usalama kushughulikia matukio haya na hata wewe kama Mkuu wa Nchi kukemea haya, hatua stahiki zichukuliwe. CHUKUA HATUA
Hii nchi chini ya utawala wa Ccm imesha laanika,
Hawajielewi.
Wewe ni wapi ulimuona rais akiwapa vijembe walio mwajiri tena kwa kiburi na dharau. Utadhani ana imbisha taarabu
 
Kumbuka wakati msamiati wa wasiojulikana ukiwa unatamba midomoni mwetu, ulikuwepo mwingine wa 'kujiteka'.

Misamiati ni mingi kwa wanaharakati lakini wapo wenye akili za kimaendeleo haya masuala ya harakati wanayasoma kwenye magazeti na kuyaacha humo humo.
Heeheeehee kujiteka? Uko serious kabisa Mkuu? Ni kesi ngapi mpaka sasa kati ya nyingi zilitoka kwa umma zilithibitika walikuwa wamejiteka?

Na hii kwa maoni yako inatosha kupuuzia mengine yote?

Hizo nchi nyingine unafikiri wanaofanya pranks na matukio ya 'kujiteka' hayatokei? Lakini wamepuuzia matukio mengine na kutochukua hatua yoyote?
 
Hii nchi chini ya utawala wa Ccm imesha laanika,
Hawajielewi.
Wewe ni wapi ulimuona rais akiwapa vijembe walio mwajiri tena kwa kiburi na dharau. Utadhani ana imbisha taarabu
Ni huzuni, ni bora angekua anatoa vijembe lakini utekelezaji unafanyika na watu hawa wanakamatwa, vijembe inaweza ikawa udhaifu wake lakini kutoa vijembe na kutofanya kitu hii inatoa picha nyingine
 
Heeheeehee kujiteka? Uko serious kabisa Mkuu? Ni kesi ngapi mpaka sasa kati ya nyingi zilitoka kwa umma zilithibitika walikuwa wamejiteka?

Na hii kwa maoni yako inatosha kupuuzia mengine yote?

Hizo nchi nyingine unafikiri wanaofanya pranks na matukio ya 'kujiteka' hayatokei? Lakini wamepuuzia matukio mengine na kutochukua hatua yoyote?
Mungu apishie mbali haya tunayoongea yasitukute. Mungu awafanyie wepesi wote waliokutwa na majanga haya.

Siasa mbaya za Mbowe na baadhi ya viongozi wa CCM za kuhubiri chuki zinatengeneza uhalisia huu wa kutisha kwa baadhi yetu.
 
Back
Top Bottom