PostGE2025 Rais Samia: Watanzania tuendelee kuliombea taifa lidumu katika amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuwasisitiza Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano viendelee kudumu nchini.
IMG-20251116-WA0045.jpg

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Jumapili, Novemba 16, 2025) alipowasilisha salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kisasa, Mkoa wa Dodoma.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimu sana. Yuko pamoja nanyi, na rai yake kwa Watanzania wote ni kuendeleza maombi kwa Taifa letu kuwa watulivu na kuiombea amani iendelee kudumu.”

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa na kuenziwa, kwa sababu pasipo amani, Taifa halitoweza kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuendesha ibada na shughuli nyingine za kijamii.

“Pasipo amani hatuwezi kutekeleza majukumu mengine yoyote, pasipo amani hatuwezi kuendesha ibada. Hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuiombea nchi yetu. Pakiwa na amani tunaweza kutekeleza yale yaliyo katika matarajio yetu, tunaweza hata kutatua yale tunayoyaona kuwa ni magumu.”

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Dkt. Christian Ndossa ambaye ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania waishi kwa kumtanguliza Mungu mbele na wawe na matumaini kwake na wajiepushe na maovu.
IMG-20251116-WA0051.jpg

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameambatana na Mwenza wake, Mama Neema Mwigulu Nchemba, katika ibada hiyo.

Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Daniel Sillo, Mbunge wa Kilolo, Ritha Kabati, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya, Mbunge wa Viti Maalumu, Balozi Dkt. Pindi Chana, Mbunge wa Itigi, Yohana Msita na Mbunge wa Kalenga, Jackson Kiswaga.
 
Attachments

  • IMG-20251116-WA0048.jpg
    IMG-20251116-WA0048.jpg
    154.8 KB · Views: 27
  • IMG-20251116-WA0052.jpg
    IMG-20251116-WA0052.jpg
    219.4 KB · Views: 32
  • IMG-20251116-WA0047.jpg
    IMG-20251116-WA0047.jpg
    185.7 KB · Views: 32
  • IMG-20251116-WA0053.jpg
    IMG-20251116-WA0053.jpg
    180.2 KB · Views: 29
  • IMG-20251116-WA0054.jpg
    IMG-20251116-WA0054.jpg
    171.5 KB · Views: 28
  • IMG-20251116-WA0050.jpg
    IMG-20251116-WA0050.jpg
    250.2 KB · Views: 29
  • IMG-20251116-WA0049.jpg
    IMG-20251116-WA0049.jpg
    205.3 KB · Views: 35
  • IMG-20251116-WA0046.jpg
    IMG-20251116-WA0046.jpg
    202.2 KB · Views: 31
Amani haitakuja kwa Maombi peke yake.Yaani watu wanauawa hakuna kuomba msamaha, hakuna kukemea wala kutake any respondibity badala yake wewe ndiye unayejifanya ni Mtoa msamaha.
 
Yeye ndo aombee amani ,nitaombeaje taifa liwe na amani wakati sihusiki katika kuiondoa amani, Samia ndo chanzo cha kupotea kwa amani Tanganyika,hivyo aombe sana yeye na sio sisi watanganyika.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuwasisitiza Watanzania waendelee kuliombea Taifa ili amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano viendelee kudumu nchini.
View attachment 3502700
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo (Jumapili, Novemba 16, 2025) alipowasilisha salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kisasa, Mkoa wa Dodoma.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawasalimu sana. Yuko pamoja nanyi, na rai yake kwa Watanzania wote ni kuendeleza maombi kwa Taifa letu kuwa watulivu na kuiombea amani iendelee kudumu.”

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha amani ya nchi inaendelea kulindwa na kuenziwa, kwa sababu pasipo amani, Taifa halitoweza kutekeleza majukumu yake ikiwemo kuendesha ibada na shughuli nyingine za kijamii.

“Pasipo amani hatuwezi kutekeleza majukumu mengine yoyote, pasipo amani hatuwezi kuendesha ibada. Hivyo ni wajibu wa kila Mtanzania kuiombea nchi yetu. Pakiwa na amani tunaweza kutekeleza yale yaliyo katika matarajio yetu, tunaweza hata kutatua yale tunayoyaona kuwa ni magumu.”

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Dkt. Christian Ndossa ambaye ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania waishi kwa kumtanguliza Mungu mbele na wawe na matumaini kwake na wajiepushe na maovu.
View attachment 3502703
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameambatana na Mwenza wake, Mama Neema Mwigulu Nchemba, katika ibada hiyo.

Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge, Daniel Sillo, Mbunge wa Kilolo, Ritha Kabati, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya, Mbunge wa Viti Maalumu, Balozi Dkt. Pindi Chana, Mbunge wa Itigi, Yohana Msita na Mbunge wa Kalenga, Jackson Kiswaga.
Wakati wanaua hawakujua hilo
 
Eeh Mungu tunaliombea taifa letu lidumu katika haki iletayo amani yako kwa wote
 
Tuombee amani ili wao waendelee kula pesa za umma bila kipingamizi
 
Watupatie miili ya wapendwa wetu kwanza tukazike ndio tuje kwenye maombi!
 
Amani haitakuja kwa Maombi peke yake.Yaani watu wanauawa hakuna kuomba msamaha, hakuna kukemea wala kutake any respondibity badala yake wewe ndiye unayejifanya ni Mtoa msamaha.
ivi kipindi cha magu mliandamana 😂
 
Anaweseseka Amani wakati ndiye ameiharibu?
Hapo ni ishara kuwa hana Amani kwa huu Ubaya uliofanywa na vikosi vya Usalama! Na Mungu anayetaka tuombe Amani anasema,(Isaya48:22)-Hapana Amani kwa Wabaya.
 
Maombi hayajawahi kuleta amani,tendeni HAKI,WAJIBIKENI nk
 
Wewe umekamata upanga kumpiga mtu halafu unasema amani?
 
Kwa hiyo Mwigulu wewe ndio umekubali kutumwa na Sa100? Je upo tiyari kubeba adhabu inayoelekezwa Juu yake?
 
Back
Top Bottom