gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,312
- 3,345
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri ya muungano wanajukwaa.
Ndugu zangu kwanza nitaanza kwa ku declear interest kwamba mimi ni mwana CCM ambae nilikuwa simuungi na sikubaliani na hayati Magufuli bila kificho kwani matendendo yake na uongozi wake haukuwa mzuri kwa maono yangu.
Kwa maono yangu awamu ya tano iliendesha nchi kimabavu pasipo kufuata utawala wa sheria sambamba na ukiukwaji wa haki za raia,uhuru wa habari uliminywa,uminywaji wa demokrasia na ukandamizwaji wa vyama vya siasa,ikiwemo na uvurugwaji wa uchumi wa raia.
Juzi mh raisi wetu mama Samia amesikika alipokuwa anaongea na wazee wa Dar es Salaam akisema amedhamiria kutatua kero zilizokuwepo na moja ya kero alizozitaja ni kukomesha pesa walizokuwa wanapokwa wafanya biashara na TRA kupitia kitengo maarufu kama task force.
Mh raisi samia si mara ya kwanza kulizungumza hili la TRA kwani nakumbuka hata siku ya kuapisha baraza lake la mawaziri alilizunguza kwa msisitizo kwamba mwenendo wa TRA si mzuri kwani imepokonya pesa wafanyabiashara kwakuwatishia kuwafungulia kesi za uhujumu uchumi.
Binafsi nimpongeze sana mh raisi kwa kuliona hili,lakini kwanini kusiundwe tume ifuatilie wale wote waliodhulumiwa pesa zao wakarudishiwa?
Mh raisi kuna wafanya biashara wengi wamekufa kwa pressure baada ya kufilisiwa na TRA,serikali ingerudisha pesa kwa wajane na watoto wa marehemu.Wapo wajane leo wameachiwa watoto na leo wanashindwa hata kulipa ada kwasababu ya dhulma za TRA.
Mh Rais kukiri kwamba kuna dhulma imetendeka halafu kusichukuliwe hatua zakuirudisha hii pesa ya dhulma kwa walengwa sio sawa.
Yote kwa yote tunafarijika sana kupata raisi mwenye hekima na busara,mh raisi hawa wachunga ng'ombe wachache wanaompinga humu mitandaoni ni vema akawapuuza.
Mungu na ambariki Rais wetu asiwe na kiburi,tambo na majigambo kwani kwa yaliyopita tumejifunza mengi.
Asante.