Mji wa Dar es Salaam ulikuwa ni sehemu tu ya mkoa wa Pwani, kutokana na idadi yake kubwa ya watu wanasiasa waliamua ujitenge ili uwe mkoa unaojitegemea. Ilala, Kinondoni, Temeke na Ubungo ilikuwa ni mitaa tu ya mji wa Dar es salaam ambayo baadae wanasiasa waliigeuza kuwa wilaya/halmashauri ili kusogeza karibu huduma kwa wananchi.
Ilala, Kinondoni na Ubungo ni mitaa/wilaya ambazo zimeshikana zinazounda jiji la Dar es Salaam, hivyo wanashirikiana kwenye mambo mengi sana ikiwemo stend kuu, mabenki, shule, nk. Hivyo kuifanya Ilala pekee kuwa jiji na nyingine kubaki kuwa halmashauri ni sawa lakini kutaleta mtafaruku wa kiutendaji muda sio mrefu ambao unaweza kusababisha Rais ajae baada ya muda wako kwisha akaamua vinginevyo tena.
Maswali tunayojiuliza wananchi ni je:
1. Mamlaka ya jiji la Ilala hayatafika kwenye halmashauri nyingine?
2. Je, Ilala, Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kinondoni zina vyanzo sawa vya mapato ya kujiendesha? Au zitagawanaje mapato?
3. Itakuwaje kama siku moja Ubungo, Temeke, Kinondoni, na Kigamboni pia zikipata hadhi ya kuwa majiji? Tutakuwa na majiji 4 yaliyoko karibu?
4. Je, jina la Dar es Salaam litatumika tukimaanisha sehemu gani kati ya hizi halmashauri?
Kwa maoni yangu mimi, kwakuwa Dar es Salaam imeungana kuanzia Kigamboni, Ilala, Ubungo na Temeke ni rahisi sana kuzivunja halmashauri zote zilizopo sasa na kulibakisha jiji la Dar es Salaam likiwa moja tu Dar es Salaam tu na kata zake ili kupunguza mzigo wa matumizi ya kuwa na wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa Wilaya, na watendaji wengine kwenye halmashuri which are more cost kuliko matumizi ya jiji bila halmashauri.
Kuvunja halmashauri zote na kubakisha jiji kunaokoa pesa nyingi zaidi kuliko kuvunja jiji na kubakisha Ilala kama jiji na halmashauri za Temeke, Ubungo, Kinondoni na kigamboni.
Kama hoja ni kubana matumizi ya uendeshaji wa Dar es Salaam basi tuvunje halmashauri zote ibaki moja tu ya jiji la Dar es Salaam na madiwani wa kuchaguliwa kwenye kata za Dar es Salaam.
Kwa kuwa tatizo la Meko ni gharama za Jiji la DAR ambalo halina ardhi, miradi wala mapato, napendekeza angefanya yafuatayo:
1. Angeacha set up iliyopo ya manispaa iendelee na pengine wazidi kuongeza manispaa zingine kama Mbagala, Pugu, Bunju. Hapa hata ile principle ya D by D (Development by Devolution) ingezidi kuwa practical.
2. Wale Mameya wa Manispaa hizo ndiyo wainde Baraza la Jiji. Kama watakuwa watano Kama zilivyo Manispaa za sasa sawa. Halafu watamchagua Mayor miongini mwao
3. Watakuwa na Sekretariati ya watu wasiozidi 5 (Katibu, Afisa Mipango, Mjasibu, Dreva, Katibu Muhtasi) ambao ndiyo watafanya kazi za uratibu
4. Concept ya wilaya ingefutwa tusiwe na ma DC kwa kuwa zile shughuli za DCs ziunganishwe kwa DEDs tu.
5. Gharama za kuendesha Sekretariati ya Jiji zitachangiwa kwa njia ya asilimia au kwa rotation ya Halmashauri moja kwa mzunguko wa mwaka mmoja mmoja
6. Ma Mayor wa kila Manispaa kupitia ma DED wao watatengeneza mipango yao na kuipitisha kwenye Halmashauri zao na Kisha zitapata endorsement ya Baraza la Jiji.
NB:
Hii ndiyo setup ya South Africa ambapo Manispaa za Soweto, Hilbrough, Kempton Park, Sandton, Randeburg, Rodeport zinasababisha JIJI moja maarufu kabisa duniani la Johannesburg
Faida za Approach Hii:
1. Ile concept ya Development by Devolution (DbD) itatekelezwa vizuri
2. Jiji la Dar es Salaam halitapoteza muendelezo wake na historia yake
3. Kutakuwa hakuna kupishana kwa mipango na maenseleo ya JIJI la Dar kwa vile mipango ya manispaa zote inaratibiwa sehemu moja
4. Kwa sasa tuna population ikadiriwayo 6 Milion. Hivyo basi tukifika mwaka 2030 Ni rahisi kuwa Mega City kwa vile population ya Jiji itafika 10 Milion