Rais, subiri kidogo kutia saini kulivunja jiji la Dar es Salaam

kwasababu mkoani daslam hakuna mji unaoitwa daslamu
Hakuna Mkoa wa dar es salaam kuna mji wa Dar es salaam, ni wanasiasa tu ambao hawakutazama mbele itakuja kutokea nini walioufanya uwe mkoa na kuchagua baadhi ya mitaa yake (Temeke, Ilala na Kinondoni) kuwa wilaya, sasa tunataka kufanya makosa mengine.
 
Natarajia wakati wetu na sisi ukifika wa kumpata Joe Biden, nina imani ndani ya siku/miezi michache tu ya uwepo wake madarakani, atabadii vitu vingi sana na kuvirejesha katika hali yake ya kawaida!!

Ngoja niwahi bookshop nikaulizie kama vile vitabu vya somo la Historia ya Tanzania vimeshatoka. Sitaki kuachwa nyuma eti! kwenye hili suala letu la UZALENDO.
 
Mkapa hakuvunja jiji, alivunja baraza la madiwani, Jiji likaongozwa na Tume badala ya Baraza

Sasa hivi limevunjwa jiji
Nyakati zinabadirika, but the same copy and paste, ila tume paste kitofauti kidogo kwasababu ya MUDA na mazingira kubadirika; enzi hizo Morogoro road ile double road ilikua inaishia Ubungo mataa but sasa hvi tunajenga 8 lanes
 
Hii anafanya kwa kumuondoa mayor wa sasa wa jiji la dar es salaam

kwa Kua Hana uwezo wa kumtumbua imebidi ageuze mchezo, sijui kamkosea nini Yule kijana
 
Mkuu ukisafiri nje ya fence ya kimawazo uliyojiwekea utaelewa kuwa councils zina peleka huduma karibu zaidi ya wananchi.

Jiji la London lina Councils 32!
Lakini hizo councils zote ziko ndani ya London kama ilivyokuwa kwa Dar es Salaam sio...
 


Hamtaki huyu omary ndio hizo vigisu zote na kumtumbua hawezi, inabidi ageuze mchezo jiwe bwana sometimes Ana Chuki za ajabu sana , sijui ni binadamu wa aina gani Yule
 
Umeongea vya maana
 
Kwa Mwanza Nyamagana pekee ndo jiji, Ilemela Manispaa na zinginezo
 
Mkoa wa Tanga kuna mji unaitwa Tanga ambao ndiyo jiji la tanga, Mkoa wa Dodoma kuna mji unaitwa Dodoma ambao ndiyo jiji la Dodoma, je mbona Mkoa wa Dar es Salam jiji lake linaitwa Ilala?
Ilala ndiyo Dar es salaam. Huko kwingine ni Temeke, kinondoni, Kigamboni, Ubungo nk
 
Kwa kuwa tatizo la Meko ni gharama za Jiji la DAR ambalo halina ardhi, miradi wala mapato, napendekeza angefanya yafuatayo:

1. Angeacha set up iliyopo ya manispaa iendelee na pengine wazidi kuongeza manispaa zingine kama Mbagala, Pugu, Bunju. Hapa hata ile principle ya D by D (Development by Devolution) ingezidi kuwa practical.

2. Wale Mameya wa Manispaa hizo ndiyo wainde Baraza la Jiji. Kama watakuwa watano Kama zilivyo Manispaa za sasa sawa. Halafu watamchagua Mayor miongini mwao

3. Watakuwa na Sekretariati ya watu wasiozidi 5 (Katibu, Afisa Mipango, Mjasibu, Dreva, Katibu Muhtasi) ambao ndiyo watafanya kazi za uratibu

4. Concept ya wilaya ingefutwa tusiwe na ma DC kwa kuwa zile shughuli za DCs ziunganishwe kwa DEDs tu.

5. Gharama za kuendesha Sekretariati ya Jiji zitachangiwa kwa njia ya asilimia au kwa rotation ya Halmashauri moja kwa mzunguko wa mwaka mmoja mmoja

6. Ma Mayor wa kila Manispaa kupitia ma DED wao watatengeneza mipango yao na kuipitisha kwenye Halmashauri zao na Kisha zitapata endorsement ya Baraza la Jiji.

NB:
Hii ndiyo setup ya South Africa ambapo Manispaa za Soweto, Hilbrough, Kempton Park, Sandton, Randeburg, Rodeport zinasababisha JIJI moja maarufu kabisa duniani la Johannesburg

Faida za Approach Hii:
1. Ile concept ya Development by Devolution (DbD) itatekelezwa vizuri

2. Jiji la Dar es Salaam halitapoteza muendelezo wake na historia yake

3. Kutakuwa hakuna kupishana kwa mipango na maenseleo ya JIJI la Dar kwa vile mipango ya manispaa zote inaratibiwa sehemu moja

4. Kwa sasa tuna population ikadiriwayo 6 Milion. Hivyo basi tukifika mwaka 2030 Ni rahisi kuwa Mega City kwa vile population ya Jiji itafika 10 Milion
 
Umeongea point sana... ila ndiyo hivyo tayari ana maamuzi yake...
 
Paragraph ya pili kutoka chini ndivyo jiji la Lagos lilivyofanya na kupata Corbunation(Jiji kubwa lililounganishwa na vitongoji vilivyosogelea jiji kuu) na kwa Dar es Salaam ni kama ulivyotaja(Mlandizi hadi Kibaha, Kisarawe, Mkuranga hadi Mwandege na Bagamoyo hadi Mapinga)
 

Dar es salaam ni mkoa kamili kiutawala, kwani RC Kunenge anatawala mkoa upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…