Rais, subiri kidogo kutia saini kulivunja jiji la Dar es Salaam

Hii anafanya kwa kumuondoa mayor wa sasa wa jiji la dar es salaam

kwa Kua Hana uwezo wa kumtumbua imebidi ageuze mchezo, sijui kamkosea nini Yule kijana
Itakuwa chaguo lake alikosa, halafu hii inakufanya uhonge watu wachache zaidi ili kumpata mlengwa wako, maana wakiwa ni madiwani wote gharama zinakuwa kubwa halafu utakuwa unabahatisha.
 
Si hiyo wilaya ya Ilala ndiyo inayobeba jiji la Dar es Salaam. Wilaya zingine zote ni manispaa.
 
Hujui complications za ki-administration na ubebaji wajibu,muingiliano wa kiutendaji na utupianaji Moira ulokuwepo maana we haupo kwenye ngazi ya utawala
Hoja ya dsm imeungana jua tuu tz bars yote imeungana! Kuna watu wamekuwa wakipigania vyeo kwajili ya ulaji kiujanja janja wamestopishwa
Mbona mikoa mingine mambo nihivyo na uongozi umekuwa rahisi? Makao makuu yamkoa ndiyo yanapewa ujiji sio mkoa mzima MF Dodoma jiji pale center lkn huko mf Kondoa kuna ujiji gani?? Mwanza jiji ukerewe kunaujiji gani?? Ilikuwa in janjajanja tuu zakutafuta mavyeo bilakazi
 
Mkoa wa Tanga kuna mji unaitwa Tanga ambao ndiyo jiji la tanga, Mkoa wa Dodoma kuna mji unaitwa Dodoma ambao ndiyo jiji la Dodoma, je mbona Mkoa wa Dar es Salam jiji lake linaitwa Ilala?
Kwani jiji la mwanza kuna wilaya/mji unaitwa mwanza ?
 
Shida unayopata tu ni kwamba kiswahili kina ishia neno Jiji lakini tukipata kiswahili cha Metropolitan basi ndio Dar es Salaam
 
Hapa pana jiji linalovunjwa na kuoteshwa jiji sehemu nyingine tuvute subira
 
Dar es salaam ni mkoa kamili kiutawala, kwani RC Kunenge anatawala mkoa upi?
Mkoa wa dsm ulipaswa kuwa unajumlisha wilaya za dsm mjini, kibaha, mkuranga, kisarawe, bagamoyo. Hivyo wilaya ya dsm ndiyo ingetakiwa iwe jiji. Lakini kusema Masaki, Mbezi Beach, Kawe, Ununio, Bunju, Chuo kikuu cha Mlimani, Mlimani City Mall na Lugalo haviko jijini ni kukaribisha mashaka yanayohitaji kufanyiwa kazi siku za usoni na watu wengine.
 
Huo mfano sio sahihi kidogo. Dar salaam ni tofauti na hiyo mikoa mingine unayoitaja. Mbeya, chunya, tukuyu, mbalali haukua mji mmoja kama ilivyo Ilala, temeke, ubungo, kinondoni. Hivyo huwezi kuita wilaya za dodoma, mpwapwa, kondoa, bahi sijui na wapi jiji la dodoma. Maana geografically ziko mbali sana. Hii ni tofauti na dar es salaam ambayo ilala, ubungo, temeke, kinondoni ambayo ilikuwa mitaa tu ndani ya mji mmoja.
 
Kwani jiji la mwanza kuna wilaya/mji unaitwa mwanza ?
Jiji la dsm ni la zamani kuliko la mwanza la juzijuzi tu, hivyo Dar es salaam haiwezi kulazimishwa ifuate na kufanana na Mwanza. Kila mji unayo historia na namna yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…