Rais TLS atoa msimamo Wakili Mpoki kufungiwa miezi 6

Rais TLS atoa msimamo Wakili Mpoki kufungiwa miezi 6

Hivi wanasheria wana mchango gani ktk uzalishaji wa nchi hii? Kazi yao ni kuzalisha migogoro ila wale bila kufanya kazi. Hiyo TLS ingefutwa tu haina faida yoyote zaidi ya kuzalisha migogoro. Kuna vitaasisi ni vya vikundi vinavyokula bila tija kwa Taifa. Sheria ni kazi ya majungu na kujionesha wanajua vifungu, hivyo vifungu vyenu vinamlisha nani. Fani zingine hazina faida hapa duniani.
Poor thinking
 
Kuna siku tutahangaika sana kupata watu waadilifu katika hii nchi.
Uko sahihi, na kadiri siku zinavyokwenda Sheria zinazidi kutekelezwa kwa utashi wa viongozi, na sio kama Sheria zilivyo. Na huu ukondoo wetu sioni ni wapi viongozi watakuwa na muda wa kutekeleza Sheria zinazowabana. Mpaka wamefikia hatua ya kutunga Sheria za kulipa wake wa wastaafu, basi Hali itazidi kuwa mbaya.
 
Hivi wanasheria wana mchango gani ktk uzalishaji wa nchi hii? Kazi yao ni kuzalisha migogoro ila wale bila kufanya kazi. Hiyo TLS ingefutwa tu haina faida yoyote zaidi ya kuzalisha migogoro. Kuna vitaasisi ni vya vikundi vinavyokula bila tija kwa Taifa. Sheria ni kazi ya majungu na kujionesha wanajua vifungu, hivyo vifungu vyenu vinamlisha nani. Fani zingine hazina faida hapa duniani.
Kwa taarifa yako kazi si lazima uzalishe bidhaa peke yake, Bali hata kutoa huduma ni kazi pia. Kwa mfano walimu wanafanya kazi, kwani ni bidhaa wanazalisha? Madaktari ni bidhaa gani wanazalisha?
 
Jaji ni mwanachama wa TLS ambayo kimsingi wanatamani utawala wa sheria unatamalaki. Lakini huyo huyo mwanachama anajikataa kutimiza wajibu wake wa kuona na kufurahia utawala wa sheria unatamalaki. Mungu wa mbinguni tuangalie sisi wajaa wako
 
Wapo wachache sana na hawana nafasi katika utumishi wa umma. Siku zinavyozidi kwenda na wakaona watu wachafu kimaadili wanabarikiwa kwa uchafu wao, wataamua kuuweka kando uadilifu wao maana haulipi katika Tanzania ya leo.
Hao unao wazungumzia hawatakuwa "waadilifu", labda kama unataka kuigeuza maana ya hilo neno.

Mtu hawezi kuacha kuwa mwadilifu kwa sababu unayoizungumzia wewe hapa.
 
Back
Top Bottom