Rais Touadera ashinda kwa Muhula wa Pili Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais Touadera ashinda kwa Muhula wa Pili Jamhuri ya Afrika ya Kati

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais Faustin-Archange Touadera ametangazwa Mshindi wa Uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 27 Desemba katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo usiku wa kuamkia leo, yamempa Touadera asilimia 53 ya kura zilizopigwa.
Mwenyekiti wa tume hiyo Mathias Morouba amesema kwa ushindi huo wa kishindo, anamtangaza Touadera kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

Morouba amesema watu wapatao 910,000 ambao ni nusu ya wote wenye sifa za kupiga kura nchini humo walijiandikisha, na kati yao asilimia 76.3 walishiriki katika zoezi la uchaguzi.

Uchaguzi huo uligubikwa na mashambulizi ya waasi watiifu kwa rais wa zamani Francois Bozize, walioazimia kuuvuruga.

Duru za hivi punde zinaarifu kuwa waasi hao wameukamata mji muhimu wa Bangassou ulio kusini mashariki, na kuwalazimisha wakaazi wake kukimbilia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 
Miss Zomboko nyanyua basi uso tukuone vizuri, sio kila siku uinamishege kichwa basi🤣🏃
 
Back
Top Bottom