Je, ni kweli Trump alitambua uwepo wa Rigathi Gachagua katika hotuba yake ya uapisho na kutoa onyo kali kwa Ruto kuhusu matukio ya Utekaji, na je, huyu Gachagua alihudhuria kwenye tukio hilo?
Your browser is not able to display this video.
Tunachokijua
Donald Trump ni Rais wa 47 wa Marekani ambaye alichaguliwa katika cheo hicho kupitia uchaguzi dhidi ya aliyekuwa makamu wa Rais Kamala Harris mwezi Novemba 2024, na kumfanya kuwa rais aliyechaguliwa kuhudumu mihula miwili isiyo isiyofuatana. Rais Trump alianza kutumikia muhula wake wa pili katika ikulu ya White House baada ya kuapishwa tarehe 20 Januari 2025 akihudumu pamoja na Seneta wa Ohio, J.D. Vance, kama Makamu wa Rais.
Kumekuwapo na Video inayosambaa sana mitandaoni ikimuonesha Rais Trump wakati wa hotuba yake baada ya kuapishwa akisema anatambua uwepo wa Rigathi GachaguaPamoja na kutoa onyo kwa Rais wa Kenya William Ruto kuhusu matukio ya Utekaji.
Je ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa kutoka kwenye video halisi iliyochapishwa na Sky News katika ukurasa wake wa mtandao wa youtube ambapo Trump alikuwa akitoa hotuba yake baada ya kuapishwa kuwa Rais wa 47 wa Marekani. Tazama video halisi hapa kuanzia dakika ya 02:04 mpaka dakika ya tatu na kuendelea.
Video hiyo imehaririwa kwa kuwekewa sauti iliyotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba huku ikiwa na mchanganyiko wa sauti halisi kutoka kwenye video halisi. Sambamba na hilo utamkaji wa maneno katika video hiyo iliyopotoshwa kwa kuzingatia mzunguko wa kinywa (lips movement) hauendani na maneno yanayosikika.
Vilevile Rigathi Gachagua hakuhudhuria hafla hiyo ya uapisho tofauti na inavyosikika katika sauti hiyo, hata hivyo siku ya tarehe 20, Januari 2025 alikuwa na kikao na baadhi ya viongozi wa jamii ya kimaasai nyumbani kwake Wamunyoro katika Kaunti ya Nyeri.
Katika video halisi iliyochapishwa na Sky News Hakuna sehemu yeyote ambayo Rais Trump amlimtaja Gachagua au Rais Ruto kuhusiana na matukio ya utekaji nchini Kenya. Sehemu ya video iliyotumika kupotosha Rais huyo wa Marekani alikuwa alikuwa akieleza namna ambavyo serikali yake itafanya mabadiliko dhidi ya mapungufu aliyoyabainisha kutoka utawala uliomaliza muda wake. Alisema;
“America will soon be stronger and far evermore exceptional than ever before, i will turn to the presidency confident and optimistic that we are at the start of the thrilling new era of nationa success. I told you of changes, sweeping the country, sunlight is pouring the entire world and America has the chance to see this opportunity like never before, but first we must be honesty about the challenges we face where they are plentiful, they will be annihilated by this great momentum that the world is now witnessing in the united states of America.
As we gather today, our government has confronted a crisis of trust for many years. A radical and corrupt establishment has extracted power and wealth from our citizens where the pillars of our society lay broken and seemingly incomplete disrepair.
Government that cannot manage even a simple crisis at home while at the same time stumbling into a continuing catalog of catastrophic events abroad it fails to protect magnificent law abiding American citizens but provide sanctuary and protection for dangerous criminals many from prisons and mental institutions that have illegally entered our country from all over the world.
Government that has given unlimited funding to the defense of foreign borders but refuses to defend American borders or more importantly its own people. Our country can no longer deliver basic services in times of emergency as recently shown by the wonderful people of North Carolina being treated so badly.”
=======
“Marekani itakuwa imara zaidi na ya kipekee, nitarejesha ujasiri na matumaini ya urais, tupo mwanzoni mwa enzi mpya ya mafanikio makubwa ya taifa. Niliwaambia kuhusu mabadiliko yatayoikumba nchi, mwanga wa jua unamulika ulimwengu mzima, na Marekani ina nafasi ya kutumia fursa hii kama haijawahi kutokea.
Lakini kwanza, tunapaswa kuwa waaminifu kuhusu changamoto tunazokabiliana nazo. Ingawa ni nyingi, zitafutwa kabisa na kasi kubwa ambayo ulimwengu sasa unaishuhudia hapa Marekani.
Tunapokusanyika leo, serikali yetu inakabiliwa na tatizo la uaminifu. Kwa miaka mingi, tabaka la uongozi lenye msimamo mkali na lililojaa ufisadi limekuwa likinyonya mamlaka na utajiri kutoka kwa raia wetu, na nguzo za jamii yetu zimevunjika na kuonekana kuwa katika hali ya kuharibika isiyorekebishika.”
“Serikali ambayo haiwezi kushughulikia hata mgogoro mdogo ndani ya nchi, huku ikijikuta ikikabiliwa na orodha inayoendelea ya matukio ya maafa nje ya mipaka yetu. Serikali hii inashindwa kuwalinda raia wake waaminifu wanaofuata sheria, lakini badala yake inatoa hifadhi na ulinzi kwa wahalifu hatari, wengi wao wakiwa wametoka magerezani na hospitali za akili, na kuingia nchini kinyume cha sheria kutoka pande zote za dunia.
Serikali ambayo inatoa fedha zisizo na kikomo kwa ajili ya kulinda mipaka ya mataifa ya kigeni, lakini inakataa kulinda mipaka ya Marekani au, watu wake wenyewe. Nchi yetu sasa imeshindwa kutoa huduma za msingi wakati wa dharura, kama ilivyooneshwa hivi karibuni kwa watu wema wa North Carolina, waliotendewa vibaya sana.”
Je, ni kweli Trump alitambua uwepo wa Rigathi Gachagua katika hotuba yake ya uapisho na kutoa onyo kali kwa Ruto kuhusu matukio ya Utekaji, na je, huyu Gachagua alihudhuria kwenye tukio hilo? View attachment 3209849 View attachment 3209826
Kama video ni genuine kwa maana kuwa ni video ambayo haijatokana na AI; basi ni maneno mazito na ya kuzingatia
Mh rais Ruto atafute muda aongee na Rais Trump kwa sababu kwenye matukio haya ya utekaji kuna aina fulani ya fabrication kwa maana kuwa yanafanywa na watu binafsi halafu inasingiziwa Serikali
Juzi tu kuna mwanaharakati mmoja Mtanzania ametekwa huko Nairobi Kenya lakini eveidence zote za utekanji huo zinapoint kwa watu binafsi walio na mlengo wa kuzichafua Seriklai za Kenya na Tanzania
Watu wa aina hii inabidi washughulikiwe kikamilifu