- Source #1
- View Source #1
Rais wa marekani Donald Trump amewasili leo mapema nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa marekani Barack Obama kufutia Taarifa za kifo cha mbwa wake mpendwa Sunny aliyekuwa akiishi ikulu ya White House kwa kipindi chote Obama alichokiwepo madarakani.
Hata hivyo familia ya Obama ilisema mazishi ya Mbwa huyo yatafanyika jumapili hii 20 Sept 2026 nyumbani kwao.
UHALISIA WA TAARIFA HII NI UPI?
Hata hivyo familia ya Obama ilisema mazishi ya Mbwa huyo yatafanyika jumapili hii 20 Sept 2026 nyumbani kwao.
UHALISIA WA TAARIFA HII NI UPI?
- Tunachokijua
- Septemba 16, 2026 Rais wa 44 wa Marekani ambaye kwa sasa ni Mstaafu, Barack Obama kupitia ukurasa wake wa X alichapisha taarifa ya masiikitiko yake na familia yake kufuatia kifo cha mbwa wao wa muda mrefu Sunny kilichotokea Septemba 15.
Kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook mtumiaji mmoja alichapisha taarifa na kueleza kuwa Rais sasa wa Marekani Donald Trump amemtembelea Obama kufuatia kufiwa na mbwa wake huyo.
JamiiCheck imefuatilia na kujirirdhisha kuwa hakuna chanzo cha kuaminika ikiwemo Ikulu ya Marekani na ukurasa wake Rasmi wa mitandao ya kijamii ikiwemo X ambayo amekuwa akiitumia mara kwa mara kutoa taarifa zake kilichomtaja Rais Trump kufika katika makazi ya Obama kufuatia kifo cha mbwa huyo.
Itakumbukwa mara kadhaa Rais Trump amekuwa akimtaja Obama kama Marais wa marekani wa hovyo kuwahi kutokea.
Rais Trump hana mahusiano mazuri na Rais Obama kiasi cha kumfanya aende kwa Rais huyo mstaafu kufuatia kifo cha mbwa wake. Amekuwa akimtaja kama Rais wa hovyo kuanzia alipoingia madarakani mwaka 2016.