SI KWELI Rais Trump amemtaka Makamu wake James Vance ajiuzulu?

SI KWELI Rais Trump amemtaka Makamu wake James Vance ajiuzulu?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
1792840991916.png
 
Tunachokijua
Donald Trump ni mwanasiasa kutokea nchini Marekani ambaye alihudumu kama Rais wa 45 wa taifa hilo na kisha kama Rais wa 47 nafasi ambayo yupo nayo hadi hivi sasa, 2026.

Makamu wa Rais Trump ni James David Vance ambaye ni makamu pia wa 50 wa taifa hilo. Mbali na siasa Vanve ni mwandishi, mfanyabiashara na mwanajeshi mstaafu wa jeshi la maji la Marekani.

Madai

Kupitia mtandao wa X kumekuwa na chapisho (Screenshot) inayodaiwa kuwa ni ya Rais wa Marekani, Donald Trump aliyoichapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa Truth Social kumtaka Vance ajiuzulu nafasi yake.

Chapisho hilo linaeleza kuwa sababu ya kufikia uamuzi huo ni kutokana na Vance kutumia majina ambayo si halisi na kwamba alizaliwa akiitwa James Donald Bowman, kisha akaenda kama James David Hamel na baadae kama James David Vance.

Uhalisia wa chapisho hilo.

Kwa kutumia ufuatiliaji kwa kutumia njia ya mtandao, JamiiCheck imejirirdhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Ufuatiliaji umebaaini kuwa chapisho hilo ni la kubuni kwa kuigizia chapisho halisi la Rais Donald Trump alikuwa akimuongelea mbunge wa Minnesota kuwa jina alilotumia kuapa nalo ambalo ni Illhan Omar si jina lake halisi.

Inaelezwa kuwa jina lake halisi ni Illhan Nur Said Elmi na hivyo Donald Trump katika chapisho lakke alimtaka kiongozi huyo ajiuzulu kutoka katika bunge la Marekani (Congress).
Back
Top Bottom